Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27 Biblia Habari Njema (BHN)

Adamu alimzaa Sethi, Sethi akamzaa Enoshi, Enoshi akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Mahalaleli, Mahalaleli akamzaa Yaredi, Yaredi akamzaa Henoki, Henoki akamzaa Methusela. Methusela alimzaa Lameki, Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Difathi na Togama. Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. Kushi alimzaa Nimrodi, aliyekuwa mtu shujaa wa kwanza duniani. Wazawa wa Misri ni Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi Wakaftori na Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti). Wana wa Kanaani walikuwa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi. Kanaani pia ndiye babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuri, Arpaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arpaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alikuwa na wana wawili; mmoja wao aliitwa Pelegi, (kwa maana wakati wake watu walikuwa wametawanyika duniani), na ndugu yake aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani. Ukoo wa Abrahamu kutokea Shemu ni kama ifuatavyo: Shemu alimzaa Arpaksadi, naye Arpaksadi akamzaa Shela. Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu; Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera, na Tera akamzaa Abramu, ambaye ndiye Abrahamu.

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Adamu, na Sethi, na Enoshi; na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; na Henoko, na Methusela, na Lameki; na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani. Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Abrahamu.

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Adamu, na Sethi, na Enoshi; na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; na Henoko, na Methusela, na Lameki; na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani. Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Ibrahimu.

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Enoki, Methusela, Lameki, Noa. Wana wa Noa walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma. Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani. Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi. Misraimu akawazaa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waariki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arfaksadi akamzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, Eberi, Pelegi, Reu, Serugi, Nahori, Tera, Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).