Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 11

11
Kuomba.
1Ikawa alipokuwa mahali akiomba, akiisha, mwanafunzi wake mmoja akamwambia: Bwana, tufundishe hata sisi kuomba, kama naye Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake!
(2-4: Mat. 6:9-13.)
2Akawaambia: Mnapoomba semeni: Baba yetu ulioko mbinguni, Jina lako litakaswe! Ufalme wako uje! Uyatakayo yatimizwe nchini, kama yanavyotimizwa mbinguni! 3Tupe kila siku chakula chetu cha kututunza! 4Tuondolee makosa yetu! Kwani nasi wenyewe humwondolea kila aliyetukosea. Usituingize majaribuni! Ila tuokoe maovuni!
5*Akawaambia: Kulikuwa na mtu mwenye rafiki; huyu akamwendea usiku wa manane na kumwambia: Rafiki yangu, unikopeshe mikate mitatu! 6Kwani rafiki yangu aliyechwelewa njiani amenifikia, nami sina cha kumwandalia. 7Basi, kwenu yule wa ndani atamjibu nini? Atamwambia: Usinisumbue! Kwani mlango umekwisha fungwa, nao watoto wangu wako kitandani pamoja nami; siwezi kuinuka, nikupe? 8Nawaambiani: Ijapo, asiinuke, ampe, kwa sababu ni rafiki yake, lakini atainuka, ampe yote yampasayo ya mgeni, kwa sababu hana soni ya kuomba.#Luk. 18:5.
(9-13: Mat. 7:7-11.)
9Nami nawaambiani: Ombeni! ndipo, mtakapopewa. Tafuteni! ndipo, mtakapoona. Pigeni hodi! ndipo, mtakapofunguliwa mlango. 10Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango. 11Tena kwenu yuko baba, mwanawe anapomwomba samaki, ampe nyoka, asimpe samaki? 12Au anapomwomba yai, ampe nge? 13Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba alioko mbinguni asizidi kuwapa Roho Mtakatifu wanaomwomba?*
Belzebuli.
(14-26: Mat. 12:22-30; 43-45; Mar. 3:22-27.)
14*Akawa akifukuza pepo aliyekuwa bubu; naye pepo alipotoka, bubu akaanza kusema. Ndipo, makundi ya watu walipostaajabu. 15Lakini walikuwako waliosema: Nguvu ya Belzebuli, mkuu wa pepo, ndiyo, anayofukuzia pepo. 16Wengine wakamjaribu wakitaka, afanye kielekezo kitokacho mbinguni.#Mar. 8:11. 17Kwa kuyajua hayo mawazo yao, akawaambia: Kila ufalme unapogombana wao kwa wao huwa mahame tu, nazo nyumba huangukiana. 18Naye Satani anapojigombanisha mwenyewe, ufalme wake utasimamikaje? Kwani mnasema: Nafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli. 19Nami nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli, Je? Wana wenu huwafukuza kwa nguvu ya nani? Kwa hiyo hao ndio watakaowaumbua. 20Lakini mimi nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya kidole cha Mungu, ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia ninyi.#2 Mose 8:19. 21Mwenye nguvu akililinda boma lake na kushika mata, basi, yaliyo yake yatakaa na kutengemana. 22Lakini mwenye nguvu kuliko yeye atakapomjia na kumshinda atamnyang'anya mata yake yote yaliyomshikiza, kisha atayagawanya mateka.#Kol. 2:15. 23Asiye wa upande wangu hunikataa; naye asiyekusanya pamoja nami hutapanya.,#Luk. 9:50. 24Pepo mchafu anapomtoka mtu hupita mahali pasipo na maji akitafuta kituo. Asipokiona husema: Nitarudi nyumbani mwangu, nilimotoka. 25Anapokuja huiona, imefagiwa na kupambwa. 26Ndipo, anapokwenda kuchukua pepo saba wengine walio wabaya kuliko yeye; nao huingia, wakae humo: hivyo ya mwisho ya mtu yule yatakuwa mabaya kuliko ya kwanza.#Yoh. 5:14.
27Ikawa, alipoyasema haya, mwanamke aliyekuwako katika kundi la watu akapaza sauti akimwambia: Lenye shangwe ni tumbo lililokuzaa na maziwa, uliyoyanyonya.#Luk. 1:28,48. 28Naye akasema: Kweli wenye shangwe ndio wanaolisikia Neno la Mungu na kulishika.*#Luk. 8:15,21.
Kielekezo cha Yona.
(29-32: Mat. 12:38-42.)
29Makundi ya watu walipomkusanyikia, akaanza kusema: Ukoo huu ni ukoo mbaya; wanatafuta kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha Yona.#Mat. 16:4; Mar. 8:12. 30Kwani kama Yona alivyowawia watu wa Niniwe kielekezo, ndivyo naye Mwana wa mtu atakavyowawia wao wa ukoo huu kielekezo. 31Yule mfalme wa kike aliyetoka kusini atawainukia waume wa ukoo huu siku ya hukumu, awaumbue. Kwani yeye alitoka mapeoni kwa nchi, aje kuusikia werevu wa Salomo uliokuwa wa kweli. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Salomo!#1 Fal. 10:1. 32Siku ya hukumu waume wa Niniwe watauinukia ukoo huu, wauumbue; kwani walijuta kwa tangazo la Yona. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Yona!#Yona 3:5. 33Hakuna mwenye kuwasha taa anayeiweka panapofichika au chini ya kapu, ila huiweka juu ya mwango, maana wanaoingia waone mwanga.#Luk. 8:16; Mat. 5:15; Mar. 4:21.
(34-36: Mat. 6:22-23.)
34Taa ya mwili ni jicho lako. Basi, jicho lako liking'aa, nao mwili wako wote unao mwanga. Lakini likiwa bovu, nao mwili wako unayo giza. 35Kwa hiyo angalia, mwanga uliomo ndani yako usiwe giza! 36Mwili wako unapokuwa wote unao mwanga, pasiwe upande wenye giza, ndipo, utakapokuwa na mwanga pia, utakuwa kama taa inayokumulikia mwanga wa umeme.
Kuwatisha Mafariseo.
37Alipokuwa katika kusema, Fariseo akamwalika chakulani. Naye akaingia, akakaa mezani.#Luk. 7:36; 14:1. 38Fariseo huyo alipoviona akastaajabu, ya kuwa hakunawa kwanza kabla ya kula.#Mat. 15:2.
(39-52: Mat. 23:1-36.)
39Bwana akamwambia: Ninyi Mafariseo, vinyweo na vyano mnaviosha nje, lakini ndani ninyi mmejaa mapokonyo na mabaya. 40M wajinga, aliyevifanya vya nje hakuvifanya vya ndani navyo? 41Basi, vile vilivyomo ndani vigawieni watu! Mara vyenu vyote huwa safi. 42Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani fungu la kumi mnalitolea hata mchicha na nyanya na mboga zo zote. Lakini penye hukumu napo penye upendo wa Mungu mnapapita. Haya yawapasa kuyashika pasipo kuyaacha yale. 43Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani nyumbani mwa kuombea mnapenda viti vya mbele, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni.#Luk. 20:46. 44Yatawapata, ninyi waandishi na Mafariseo, kwani mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu hukanyaga juu yao, wasiyajue.
45Ndipo, mjuzi wa Maonyo alipojibu akimwambia: Mfunzi, ukisema hayo unatutukana hata sisi. 46Naye akasema: Nanyi wajuzi wa Maonyo yatawapata, kwani mnatwika watu mizigo isiyochukulika, nanyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kidole chenu kimoja tu. 47Yatawapata ninyi, kwani mnayajenga makaburi ya wafumbuaji, nao baba zenu ndio waliowaua. 48Hivyo mnayashuhudia matendo ya baba zenu, ya kuwa yanawapendeza; kwani wale waliwaua, nanyi mnawajengea. 49Kwa sababu hii ujuzi wa Mungu ulisema: Nitatuma kwao wafumbuaji na mitume, wengine wao watawaua, wengine watawafukuza, 50wao wa kizazi hiki walipishwe damu za wafuambji wote zilizomwagwa tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa, 51kuanzia damu ya Abeli mpaka kuifikia damu ya Zakaria aliyeuawa katikati ya meza ya Bwana na Nyumba ya Mungu. Kweli nawaambiani: Wao wa kizazi hiki watazilipa.#1 Mose 4:8; 2 Mambo 24:20-21. 52Yatawapata, ninyi wajuzi wa Maonyo, kwani mliutwaa ufunguo wa utambuzi; wenyewe hamkuingia, mkawazuia wao waliotaka kuingia.
53Alipotoka mle, waandishi na Mafariseo wakaanza kumtunduia sana na kumwuliza maneno mengi 54na kumnyatia wakiwinda maneno, anayoyasema, kama wataona la kumsuta.#Luk. 20:20.

Iliyochaguliwa sasa

Luka 11: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia