Luka 10
10
Kutuma mitume 70.
(1-12: Mat. 10,7-16.)
1Kisha Bwana akachagua wengine 70, akawatanguliza mbele yake wawiliwawili, waingie kila mji na kila mahali, alipotaka kwenda mwenyewe. 2Naye akawaambia: Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Mwombeni mwenye mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake! 3Nendeni! Tazameni, nawatuma ninyi, mwe kama wana kondoo walio katikati ya mbwa wa mwitu! 4Msitwae mfuko wala mkoba wala viatu! Tena msiamkiane na mtu njiani! 5Lakini nyumbani mo mote, mtakamoingia, kwanza semine: Nyumba hii itengemane! 6Itakapokuwa, yumo mwenye kutengemana, utengemano wenu utamkalia. Lakini kama hatakuwamo, utawarudia ninyi. 7Namo nyumbani mlemle mkaeni mkila, mkinywa mnavyopewa! Kwani mtenda kazi hupaswa na kupewa mshahara wake. Msizunguke nyumba kwa nyumba! 8Namo mjini mo mote, mtakamoingia, nao wakiwapokea, vileni, mnavyoandaliwa! 9Waponyeni wagonjwa waliomo nakuwaambia: Ufalme wa Mungu umewakaribia! 10Lakini mjini mo mote, mtakamoingia, wasipowapokea, tokeni Lakini mjini mo mote, mtakamoingia, wasipowapokea, tokeni mwao, mwende uwanjani mkisema: 11Hata mavumbi ya mji wenu yaliyotushika miguuni twawakung'utia ninyi; lakini haya yatambueni: Ufalme wa Mungu umekaribia! 12Nawaambiani: Siku ile mji wa Sodomu utapata mepesi kuliko mji ule. 13Yatakupata, wewe Korasini! Yatakupata, wewe Beti-Saida! Kwani ya nguvu yaliyofanyika kwenu kama yangalifanyika Tiro na Sidoni, wangalijuta kale na kujivika magunia na kujikalisha majivuni. 14Lakini penye hukumu miji ya Tiro na Sidoni itapata machungu yaliyoi madogo kuliko yenu. 15Nawe Kapernaumu, hukupazwa mpaka mbinguni? Utatumbukia mpaka kuzimuni. 16Anayewasikia ninyi hunisikia mimi. Naye anayewatengua ninyi hunitengua mimi. Naye anayenitengua mimi humtengua naye aliyenituma.
Kurudi kwao mitume 70.
17*Wale 70 wakarudi wenye furaha, wakasema: Bwana, hata pepo hututii kwa Jina lako. 18Ndipo, alipowaambia: Nalimwona Satani, akianguka kama umeme toka mbinguni. 19Tazameni, nimewapa nguvu za kukanyaga nyoka na nge, mshinde uwezo wote wa yule mchukivu, tena hakuna kitu kitakachowapotoa. 20Lakini msiyafurahie hayo, ya kuwa pepo huwatii, ila yafurahieni, ya kuwa mmeandikwa majina yenu mbinguni!*
(21-22: Mat. 11,25-27.)
21Saa ileile Roho Mtakatifu akamshangiliza, naye akasema: Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwani hayo umewaficha werevu na watambuzi, ukawafunulia wachanga. Ndio, Baba, kwani hivyo ndivyo, ulivyopendezwa navyo. 22Vyote nimepewa na Baba yangu. Hakuna anayemtumbua Mwana, kama ni nani, pasipo Baba; wala hakuna anayemtambua Baba, kama ni nani, pasipo Mwana, na kila, Mwana atakayemfunulia.
23*Akawapindukia wanafunzi, akawaambia, walipokuwa peke dyao: Yenye shangwe ni macho yanayoyaona, mnayoyaona ninyi. 24Kwani nawaambiani: Wengi waliokuwa wafumbuaji na wafalme walitaka kuyaona, mnayoyaona ninyi, lakini hawakuyaona; walitaka kuyasikia, mnayoyasikia ninyi, lakini hawakuyasikia.
Msamaria mwenye huruma.
(25-28: Mat. 22,35-40; Mar. 12,28-34.)
25Pakawapo mjuzi wa Maonyo, akainuka, akamtega akisema: Mfunzi, nifanye nini, nipate kuurithi uzima wa kale na kale? 26Naye akamwambia: Katika Maonyo imeandikwa nini? Unasomaje? 27Akajibu akisema: Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu yako yote na kwa mawazo yako yote! Naye mwenzio umpende, kama unavyojipenda mwenyewe! 28Akamwambia: Umejibu kweli; yafanye hayo! Ndipo, utakapopata kuishi. 29Lakini kwa sababu alitaka kujijulisha kuwa ni mwongofu, akamwambia Yesu: Mwenzangu ni nani? 30Yesu akalishika neno hili akisema: Kulikuwa na mtu, alitoka Yerusalemu, akatelemka kwenda Yeriko, akaguiwa na wanyang'anyi. Hao walipokwisha kumvua nguo zake, na kumpiga vigongo, wakaenda zao na kumwacha, akitaka kufa. 31Ikatukia, mtambikaji akiitelemkia njia ile; alipomwona akaepuka, akapita. 32Vilevile hata Mlawi akafika mahali pale; lakini alipomwona akaepuka, akapita. 33Kisha Msamaria aliyeifuata njia ile akaja huko, alikokuwa; alipomwona akamwonea uchungu, 34akamjia, akamfunga madonda yake akiyamwagia mafuta na mvinyo, akampandisha juu ya punda wake yeye mwenyewe, akampeleka kifikioni, akamwuguza. 35Siku ya kesho akatoa shilingi mbili, akampa mwenye fikio, akasema: Mwuguze huyu! Kama unatumia kuzipita hizi, nitakulipa zote nitakaporudi. 36Waonaje? Katika hao watatu aliyejifanya kuwa mwenzake yule aliyeguiwa na wanyang'anyi ni yupi? 37Naye akasema: Ndiye aliyemwonea huruma. Ndipo, Yesu alipomwambia: Nenda nawe, ufanye vivyo hivyo!*
Maria na Marta.
38*Walipokwenda zao, akaingia kijijini. Mlikuwa na mwanamke, jina lake Marta, akamfikiza nyumbani mwake. 39Naye alikuwa na ndugu yake aliyeitwa Maria; huyu akajiketisha miguuni pa Bwana, akamsikiliza maneno yake. 40Lakini Marta akabururwa huko na huko kwa utumikizi mwingi. Kisha akaja kusimama hapo, alipokuwa, akasema: Bwana, huvitazami, huyu ndugu yangu akiniacha, nitumike peke yangu? Umwambie, anisaidie! 41Lakini Bwana akajibu akimwambia: Marta, Marta, unahangaika kwa kusumbukia mambo mengi. 42Lakini vinavyopasa ni vichache au kimoja tu. Maria amelichagua fungu lililo jema, naye hatapokwa.*
Iliyochaguliwa sasa
Luka 10: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.