Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 9

9
Sauli anakwenda Damasko.
(1-22: Tume. 22:3-16; 26:9-18.)
1Naye Sauli alikuwa akingali bado akiwatolea wanafunzi wa Bwana ukorofi kwa kuwatisha na kwa kuwaua. Akamwendea mtambikaji mkuu,#Tume. 8:3. 2akataka kwake barua za kwenda Damasko, aende nazo kwenye nyumba za kuombea za Wayuda, kwa maana alitaka kuwafunga na kuwapeleka Yerusalemu wo wote, atakaowaona wa njia hiyo, wakiwa waume au wake. 3Lakini alipokuwa akienda na kufika karibu ya Damasko, mara akamulikiwa na mwanga uliotoka mbinguni,#Tume. 22:3-21; 26:9-20; 1 Kor. 15:8. 4akaanguka chini, akasikia sauti iliyomwambia: Sauli, Sauli, unanifukuzaje? 5Alipouliza: Ndiwe nani, Bwana? akajibu: Mimi ni Yesu, ambaye unanifukuza wewe.#Tume. 5:39. 6Utashindwa na kupiga mateke penye machomeo. Lakini inuka, uingie mjini! Ndimo, utakamoambiwa yakupasayo, uyafanye. 7Lakini wenziwe waliokuwa pamoja naye njiani walikuwa wamesimama, wasiweze kusema, kwa sababu waliusikia uvumi, wasione mtu. 8Sauli alipoinuka chini, macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; kwa hiyo wakamshika mkono, wakampeleka Damasko. 9Siku tatu akawapo, asione kitu, wala asile, wala asinywe.
Sauli na Anania.
10Mlikuwa na mwanafunzi mle Damasko, jina lake Anania. Huyo Bwana akamwambia katika njozi: Anania! Aliposema: Tazama, nipo hapa Bwana! 11Bwana akamwambia: Inuka, uende kufika penye barabara inayoitwa Nyofu, uulize nyumbani mwa Yuda, kama yumo mtu wa Tarso, jina lake Sauli. Kwani tazama, yumo katika kuomba.#Tume. 21:39. 12Naye ameona mtu, jina lake Anania, anavyoingia humo, alimo, ambandikie mikono, apate kuona tena. 13Anania akajibu: Bwana, nimesikia kwa watu wengi maovu yote, mtu huyo aliyowafanyia watakatifu wako walioko Yerusalemu. 14Tena amepata ruhusa kwa watambikaji wakuu kuwafunga hapa wote pia wanaolitambikia Jina lako.#1 Kor. 1:2. 15Lakini Bwana akamwambia: Nenda tu! Kwani mtu huyu ataniwia chombo kiteule cha kulipeleka Jina langu mbele yao wamizimu na wafalme na wana wa Isiraeli.#Tume. 13:46; 25:13; 27:24; Rom. 1:5; Gal. 1:15-16. 16Nami nitamwonyesha mateso yote, atakayoteswa kwa ajili ya Jina langu.#Tume. 9:23-29; 2 Kor. 11:23-28. 17Kisha Anania akaondoka, akaenda, akaingia nyumbani mle, akambandikia mikono akisema: Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekuotokea njiani, alipokuja, amenituma, upate kuona tena na kujazwa Roho takatifu. 18Papo hapo pakawa kama magamba yaliyoanguka toka machoni pake, akaona, tena akainuka, akabatizwa. 19Naye alipokwisha kula chakula akapata nguvu tena. Akakaa siku kidogo, pamoja na wanafunzi waliokuwamo Damasko, 20hakukawia kuipiga mbiu ya Yesu katika nyumba za kuombea akisema: Huyo ndiye Mwana wa Mungu. 21Wote waliomsikia wakahangaika mioyoni, wakasema: Je? Huyu siye aliyekuwa akiwateka Yerusalemu waliolitambikia Jina hili? Huku nako hakuyajia yayo hayo kuwafunga na kuwapeleka kwa watambikaji wakuu?#Tume. 8:1; 9:1,14; 26:10. 22Lakini Sauli akakaza kutenda nguvu, akawatatanisha Wayuda waliokaa Damasko akiwashinda kwa kusema: Huyu ndiye Kristo.#Tume. 18:28.
Kukimbia kwake Sauli.
23Siku zilipokwisha pita nyingi, Wayuda wakala njama ya kumwangamiza, 24lakini Sauli alipata kuitambua njama yao. Walipomwotea malangoni pa mji mchana na usiku, wapate kumwangamiza, 25ndipo, wanafuanzi walipomchukua usiku, wakamtia kapuni, wakamshusha ukutani.#2 Kor. 11:32-33.
26Alipofika Yerusalemu akajaribu kugandamiana na wanafunzi, wote wakiwa wakingali na woga wa kumwogopa, wasiitikie, ya kuwa ni mwanafunzi;#Gal. 1:17-19. 27ndipo, Barnaba alipomchukua, akampeleka kwa mitume, akawasimulia, alivyomwona Bwana njiani, navyo alivyosema naye, tena alivyolitangaza Jina la Yesu huko Damasko waziwazi.#Tume. 9:20. 28Kisha akafuatana nao akiingia, tena akitoka nao Yerusalemu, akalitangaza Jina la Bwana waziwazi. 29Hata Wayuda waliotoka Ugriki akasema nao na kubishana nao. Ndipo, walipotafuta njia ya kumwangamiza. 30Lakini ndugu walipoyatambua wakamsindikiza mpaka Kesaria, wakamtuma kwenda zake Tarso.#Tume. 11:25; Gal. 1:21.
Petero katika Lida na Yope.
31Hivyo wateule walitengamana pote katika Yudea na Galilea na Samaria, wakajijenga, wakaendeleana kwa kumcha Bwana, tena wakawa wengi wakitulizwa na Roho Mtakatifu. 32Ikawa, Petero alipopita pote akashuka na kuwafikia hata watakatifu waliokaa Lida. 33Huko akaona mtu, jina lake Enea, alikuwa amepooza na kulala kitandani miaka minane. 34Petero akamwambia: Enea, Yesu Kristo anakuponya; inuka, ujitandikie mwenyewe! Papo hapo akainuka. 35Walipomwona wao wote waliokaa Lida na Saroni, wakageuka, wamfuate Bwana.
36Yope mlikuwamo mwanafunzi mwanamke, jina lake Tabea, maana yake ni Paa. Huyu alikuwa na matendo mema mengi ya kugawia wengi. 37Ikawa, siku zile akaugua, akafa; kisha wakamwosha, wakamlaza katika chumba cha juu. 38Kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu ya Yope, wanafunzi walisikia, ya kuwa Petero yuko huko; kwa hiyo wakatuma kwake watu wawili, wamwombe, asikawie kuja kwao. 39Petero akainuka, akaenda nao. Alipofika, wakapanda naye kwenda katika chumba cha juu. Humo wanawake wajane wote wakamjia, wakasimama wakilia na kumwonyesha kanzu na nguo zote, alizowashonea yule Paa alipokuwa pamoja nao. 40Petero akawatoa wote, waje nje, akapiga magoti, akamwomba Mungu na kuugeukia ule mwili wake, akasema: Tabea, inuka! Ndipo, alipoyafumbua macho yake; alipomwona Petero akajiketisha.#Mar. 5:41. 41Naye akamshika mkono, akamwinua, akawaita wale watakatifu na wale wajane, akamsimamisha mbele yao, akiwa yu hai.#Tume. 9:32. 42Vikaja kutambulikana Yope mjini mote; kwa hiyo wengi wakamtegemea Bwana. 43Akakaa siku nyingi huko Yope kwa fundi wa kutengeneza ngozi, jina lake Simoni.#Tume. 10:6.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 9: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia