Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 8

8
Mafukuzo ya Wakristo.
1Sauli naye alikuwa amependezwa na kuuawa kwake. Siku ile wateule waliokuwamo Yerusalemu wakashambuliwa na kufukuzwa kabisa; kwa hiyo wote wakatawanyika katika nchi za Yudea na za Samaria; waliosalia ni mitume tu.#Tume. 7:58; 11:19. 2Ndipo, watu wengine wenye kumcha Mungu walipomzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.#Mat. 14:12. 3Lakini Sauli akawajengua wateule, akaingia nyumba kwa nyumba, akawakokota waume na wanawake, akawatia kifungoni.#Tume. 9:1; 22:4.
Filipo.
4Wale waliotawanyika wakapita huko na huko wakiipiga mbiu njema ya lile Neno. 5Filipo akashuka kuuingia mji wa Samaria, akawapigia mbiu ya Kristo;#Tume. 6:5. 6watu wengi wakashikamana na yale yaliyosemwa na Filipo, mioyo yao ikawa mmoja tu kwa hayo, waliyoyasikia na kuviona vielekezo, alivyovifanya. 7Kwani wengi waliopagawa na pepo wachafu walitokwa nao, wakipiga makelele makubwa, hata wengi waliokuwa wenye kupooza na viwete wakapona.#Mar. 16:17. 8Mjini mle mkawa na furaha nyingi.#Yoh. 4:40-42.
Mganga Simoni.
9Kulikuwa na mtu mjini mle, jina lake Simoni, aliyekuwa akiwahangaisha watu wote wa Samaria kwa uganga wake akijisemea mwenyewe: Mimi ni mwenye uwezo. 10Wote, wadogo hata wakubwa, wakashikamana naye wakisema: Huyu ndio uwezo wa Mungu unaoitwa mkuu. 11Lakini walishikamana naye, kwa sababu aliwahangaisha siku nyingi kwa uganga wake. 12Lakini walipomtegemea Filipo aliyewapigia mbiu njema ya ufalme wa Mungu na ya Jina la Yesu Kristo, wakabatizwa, waume na wake.#Mat. 28:19. 13Hata Simoni mwenyewe akamtegemea Mungu, akabatizwa, akashikamana na Filipo; alipoona vielekezo na matendo makuu ya nguvu yaliyofanyizwa naye akahangaika moyoni.
14Mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia, ya kuwa Wasamaria wamelipokea Neno la Mungu, wakamtuma Petero na Yohana, waende kwao. 15Nao wakashuka, wakawaombea, wapewe Roho takatifu. 16Kwani kwao hakuna hata mmoja aliyeshukiwa nayo, walikuwa wamebatiziwa tu Jina la Bwana Yesu. 17Papo hapo, wale walipowabandikia mikono, walipewa Roho takatifu. 18Lakini Simoni alipoona, ya kuwa watu hupewa Roho, mitume wakiwabandikia mikono, akawaletea fedha, 19akasema: Nipeni nami nguvu hii, mtu nitakayembandikia mikono apewe Roho takatifu! 20Lakini Petero akamwambia: Fedha zako na ziangamie pamoja na wewe, kwa sababu umewaza, ya kuwa gawio lake Mungu linanunulika kwa mali! 21Wewe jambo hili hugawiwi hata kifungu tu, kwani moyo wako haukunyoka mbele ya Mungu. 22Sharti ujute na kuuacha huu uovu wako, ukimwomba Bwana, labda utapata kuondolewa mawazo ya moyo wako. 23Kwani nakuona, unayo yaliyo machungu kama nyongo, tena u mtumwa wa upotovu. 24Ndipo, Simoni alipojibu akisema: Niombeeni ninyi kwa Bwana mambo hayo, mliyoyasema, yasinipate hata moja! 25Walipokwisha kulishuhudia Neno la Bwana na kulisema po pote wakarudi kwenda Yerusalemu wakiipiga hiyo mbiu njema katika vijiji vingi vya Wasamaria.
Mtunza mali wa mfalme wa kike Kandake.
26*Malaika wa Bwana akamwambia Filipo akisema: Inuka, uende upande wa kusini, uifuate barabara itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza, ileile iliyokwisha kufa. 27Ndipo, alipoinuka akaenda. Mara akaona mtu wa Etiopia; huyu alikuwa mtunza mali na mtu mwenye nguvu wa Kandake, mfalme wa kike wa Etiopia, alizisimamia mali zake zote. Alikuwa amekwenda Yerusalemu kula sikukuu. 28Lakini alipokuwa anarudi na kukaa garini mwake alikisoma kitabu cha mfumbuaji Yesaya. 29Ndipo, Roho alipomwambia Filipo: Haya! Lijongelee gari hili, ulifuatefuate! 30Filipo akamwendea mbio, akamsikia, alivyokisoma kitabu cha mfumbuaji Yesaya; alipomwuliza: Unayatambua, unayoyasoma? 31akasema: Nitawezaje, mtu asiponiongoza? akambembeleza Filipo, apande, akae pamoja naye. 32Nalo fungu la Maandiko, alilolisoma, lilikuwa hili:
Kama kondoo alipelekwa kuchinjwa;
kama mwana kondoo anavyomnyamazia
mwenye kumkata manyoya,
vivyo hivyo naye hakukifumbua kinywa chake.#Yes. 53:7-8.
33Kwa hivyo, alivyonyenyekea, alinyimwa uamuzi mnyofu;
yuko nani atakayesimulia, ukoo wake ulivyokuwa?
Kwani ameondolewa katika nchi yao walio hai, asikae nchini.
34Mtunza mali akamwuliza Filipo akisema: Nakuomba, uniambie: Haya mfumbuaji anayasema ya nani? Anajisema mwenyewe au anamsema mwingine? 35Ndipo, Filipo alipokifumbua kinywa chake, akaanza kwa Maandiko yale yale akimpigia mbiu ya Yesu. 36Walipoendelea njiani wakafika penye maji kidogo, mtunza mali akasema: Tazama, yako maji, iko nini tena inayozuia, nisibatizwe? 37Filipo akasema: Ukimtegemea Bwana kwa moyo wako wote, inawezekana. Ndipo, alipojibu akisema: Namtegemea Yesu Kristo kuwa Mwana wake Mungu;#Mat. 16:16; Mat. 16:16. 38kisha akaagiza, gari lisimame, wakashuka wote wawili majini, Filipo na mtunza mali, akambatiza.* 39Lakini walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana alimpokonya Filipo, mtunza mali asimwone tena. Kisha akaishika njia yake na kufurahi.#1 Fal. 18:12. 40Lakini Filipo akaonekana Asdodi akiipiga hiyo mbiu njema katika miji yote, aliyoipita, hata akafika Kesaria.#Tume. 21:8-9.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 8: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia