Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 5

5
Anania na Safira.
1Kulikuwa na mtu jina lake Anania, na mkewe Safira; huyu alipouza kiunga 2akaficha fungu la fedha, alizozipata, naye mkewe alivijua. Kisha akaleta fungu moja, akaliweka miguuni pa mitume.#Tume. 4:37. 3Lakini Petero akasema: Anania, mbona Satani ameenea moyoni mwako, ukamdanganya Roho Mtakatifu na kuficha fungu la fedha za kiunga?#Yoh. 13:2. 4Hakikuwa mali yako, uliyoweza kukaa nayo? Hata kilipokwisha kuuzwa, je? Hukuweza kufanya, kama ulivyopenda? Mbona umelitia jambo hilo moyoni mwako? Hukudanganya watu, ila umemdanganya Mungu. 5Anania alipoyasikia maneno haya akaanguka chini, akakata roho. Ndipo, woga mwingi ulipowaingia wote walioyasikia. 6Kisha vijana wakainuka, wakamfunga nguo, wakampeleka nje, wakamzika.
7Zilipopita kama saa tatu, mkewe akaingia, asiyajue yaliyofanyika. 8Petero akamwuliza: Niambie: Fedha, mlizozipata kwa kukiuza kiunga, ndizo hizi? Naye aliposema: Ndio, ni zizi hizi, 9Petero akamwambia: Mbona ninyi mmepatana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama, miguu yao waliomzika mumeo iko nje mlangoni, watakupeleka wewe nawe! 10Papo hapo akaanguka chini miguuni pake, akakata roho. Wale vijana walipoingia na kumkuta, amekufa, wakampeleka nje, wakamzika hapo pa mumewe. 11Ndipo, woga mwingi ulipowaingia wateule wote nao wote walioyasikia haya.
Vioja
12Vikafanyika vielekezo na vioja vingi kwa mikono ya mitume kwa watu wa kwao, wale wote wakiwa pamoja katika ukumbi wa Salomo, kwa sababu mioyo yao ilikuwa ilikuwa mmoja.#Tume. 3:11. 13Lakini wengine hakuna hata mmoja aliyejipa moyo na kugandamiana nao, maana watu waliwakuza. 14Nao waliomtegemea Bwana wakaongezeka sana, ni vikundi vizima vya wanaume na vya wanawake.#Tume. 2:47; 6:7. 15Kwa hiyo watu wakawatoa hata wagonjwa, wakawaweka njiani, wakilala vitandani au majamvini, kwamba Petero akipita, kivuli chake tu kiwafikie mmojammoja.#Tume. 19:11-12. 16Wakakusanyika hata watu wengi wa vijiji vilivyouzunguka Yerusalemu, wakaleta wagonjwa nao wenye kupagawa na pepo wachafu, wakaponywa wote.
Mitume mbele ya wakuu.
17Pakainuka mtambikaji mkuu nao wote waliokuwa naye, ndio wa chama kile cha Masadukeo; kwa kujaa wivu#Tume. 4:1,6. 18wakawakamata mitume, wakawafunga na kuwapeleka kifungoni. 19Lakini usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya kifungoni, akawatoa, akasema:#Tume. 12:7. 20Nendeni, msimame Patakatifu kuwaambia watu wa kwenu maneno yote ya uzima huo! 21Walipoyasikia haya wakapaingia Patakatifu, kulipokucha, wakafundisha. Lakini mtambikaji mkuu nao waliokuwa pamoja naye wakaja, wakawakusanya wenzao wakuu na wazee wote wa wana wa Isiraeli, wakatuma watu bomani, wawalete. 22Hao watumishi walipofika hawakuwaona kifungoni, wakarudi, wakaleta habari 23wakisema: Kifungo tumekikuta, kimefungwa vizuri na kukazwa sana, hata walinzi tuliwaona, wamesimama milangoni; lakini tulipofungua hatukuona mtu ndani. 24Mlinda Patakafitu nao watambikaji wakuu walipoyasikia maneno haya wakahangaika sana, wasijue, jambo hilo litakavyokuwa. 25Pakaja mtu, akawasimulia: Tazameni, watu hao, mliowatia kifungoni, wamo nyumbani mwa Patakatifu, wamesimama na kufundisha watu!
26Ndipo, mlinda Patakatifu alipokwenda na watumishi, akawaleta, lakini si kwa nguvu, kwani waliwaogopa watu, wasije, wakawapiga mawe. 27Walipowaleta, wakawasimamisha mbele yao wakuu. Mtambikaji mkuu akawauliza: 28Hatukuwakemea kwa nguvu ya kwamba: Msifundishe mambo ya Jina hilo? Lakini tazameni, mafundisho yenu mmeyaeneza Yerusalemu, tena mwataka kutusingizia damu ya mtu yule.#Tume. 4:18; Mat. 27:25. 29Ndipo, Petero na mitume walipojibu wakisema: Sharti tumtii Mungu kuliko watu!#Tume. 4:19; Dan. 3:18. 30Mungu wa baba zetu amemfufua Yesu, mliyemwua ninyi na kumtundika mtini;#Tume. 3:15. 31huyo ndiye, Mungu aliyempaza na kumketisha kuumeni kwake, awe kiongozi na mponya, ajutishe Waisiraeli, wapate kuondolewa makosa.#Tume. 2:33. 32Nasi ndio mashahidi wa mambo hayo pamoja na Roho Mtakatifu, Mungu aliyewapa wale waliomtii.#Luk. 24:48; Yoh. 15:26-27. 33Walipoyasikia haya wakakereza meno, wakataka kuwaua.#Tume. 7:54.
34*Kisha pakainuka hapo penye wakuu Fariseo, jina lake Gamalieli; ni mfunzi wa Maonyo mwenye cheo kwa watu wote, akaagiza, wale watu wapelekwe nje kidogo.#Tume. 22:3. 35Kisha akawaambia: Waume Waisiraeli, jilindeni kwa ajili ya hayo, mtakayowatendea watu hawa! 36Kwani mbele ya siku hizi aliondokea Teuda, akajiwazia, kwamba yeye ndiye mtu, nao watu waliomfuata wakapata kama 400. Alipouawa, wote waliomtii wakatawanyika, wakapoteapotea, tena hakuna kitu. 37Kisha katika siku za kuandikiwa kodi aliondokea Yuda Mgalilea, akatenga kikundi cha watu, wamfuate yeye. Naye alipoangamia, wote waliomtii wakatawanyika nao. 38Kwa hiyo sasa nawaambiani: Mtengamane na watu hawa, mwaache! Kwani mawazo hayo au kazi hizo zikiwa zimetoka kwa watu zitakoma;#Mat. 15:13. 39lakini zikiwa zimetoka kwake Mungu, hamwezi kuwakomesha, msije mkaonekana, ya kuwa mnagombana na Mungu.#Tume. 9:5. 40Ndipo, walipomwitikia, wakawaita wale mitume, wakawapiga, wakawakemea, wasiseme tena mambo ya Jina la Yesu, kisha wakawafungua.#Tume. 22:19. 41Wao wakatoka machoni pa wakuu wakichangamka, kwa sababu Mungu amewapa kutwezwa kwa ajili ya Jina lake.#Mat. 5:10-12; 1 Petr. 4:13. 42Siku zote hawakuacha kufundisha na kuutangaza Utume mwema wa Yesu Kristo hapo Patakatifu na nyumbani mo mote.*

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 5: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia