Matendo ya Mitume 6
6
Kuchaguliwa kwa wasaidiaji saba.
1Siku zile wanafunzi walipozidi kuwa wengi, Wagriki waliwanung'unikia Waebureo, kwani wanawake wajane wa kwao hawakutumikiwa kama wengine na kugawiwa kila siku vilivyowapasa.#Tume. 4:35. 2Hapo wale kumi na wawili wakawakusanya wingi wa wanafunzi, wakasema: Haifai, sisi tukiliacha Neno la Mungu, tutumikie mezani. 3Ndugu zetu, mkague watu saba wa kwenu wanaojulikana, ya kuwa wamejaa Roho na werevu wa kweli, tuwaweke, walitumikie jambo hilo!#1 Tim. 3:7-9. 4Lakini sisi tuishike kazi yetu ya kuomba na kulitumikia Neno. 5Neno hili likawapendeza wale wote waliokuwako, wakamchagua Stefano aliyekuwa mwenye kumtegemea Bwana kwa moyo wote na mwenye Roho takatifu na Filipo na Porokoro na Nikanoro na Timoni na Parmena na Nikolao aliyekuwa mfuasi wa Kiyuda wa Antiokia.#Tume. 8:5. 6Hawa ndio, waliowasimamisha mbele ya mitume, wakawabandikia mikono wakiwaombea kwa Mungu.#Tume. 1:24; 13:3; 14:23. 7Hivyo Neno la Mungu likaendelea, wanafunzi wakapata kuwa wengi sana Yerusalemu, hata watambikaji wengi wakamtegemea Bwana na kumtii.#Tume. 19:20.
Stefano
8Naye Stefano alikuwa mwenye nguvu nyingi za kumtegemea Bwana, akafanya vioja na vielekezo vikubwa mbele ya watu. 9Kwa hiyo wakainuka wengine waliokuwa wa chama kilichoitwa cha Walibertino na watu wa Kirene na wa Alekisandria nao walitoka Kilikia na Asia, wakaulizana na Stefano. 10Lakini hawakuweza kuyabisha, aliyoyasema kwa werevu uliokuwa wa kweli na kwa Roho.#Luk. 21:15. 11Ndipo, walipoleta watu wengine waliosema: Tumemsikia, alivyosema maneno ya kumbeza Mose na Mungu.#Mat. 26:60-66. 12Wakawachafua watu na wazee na waandishi, wakamjia, wakamkamata, wakampeleka barazani kwa wakuu. 13Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema: Mtu huyu haachi kusema maneno ya kupakataa mahali Patakatifu, hata maonyo.#Yer. 26:11. 14Kwani tumesikia, alivyosema: Yesu wa Nasareti atapabomoa mahali hapa na kuzigeuza desturi, Mose alizotupa. 15Ndipo, wote waliokaa barazani kwa wakuu walipomkazia macho, wakauona uso wake kuwa kama uso wa malaika.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo ya Mitume 6: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.