Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 17

17
Tesalonike na Beroya.
1Wakapita katika Amfipoli na Apolonia, wakafika Tesalonike palipokuwa na nyumba ya kuombea ya Wayuda.#1 Tes. 2:2. 2Kama Paulo alivyozoea, akaingia humo, akaongea nao maneno ya Maandiko siku tatu za mapumziko. 3Akawafunulia na kuwaelezea, ya kuwa Kristo alipaswa na kuteswa na kufufuka katika wafu, akawaambia: Yesu, ambaye ninawatangazia habari zake, yuyu huyu ndiye Kristo.#Luk. 24:26-27,45-46. 4Wamoja wao wakashindwa mioyoni, wakashikamana nao akina Paulo na Sila; nao waliotoka kwa Wagriki wenye kumcha Mungu walikuwa wengi mno, hata wanawake wenye cheo hawakuwa wachache. 5Lakini Wayuda wakaingiwa na wivu, wakajichukulia kikundi cha majitu mabaya wasiokuwa na kazi; hao wakakusanya kundi zima la watu, kisha wakauchafua mji wote, wakaisogeleasogelea nyumba ya Yasoni, wakawatafuta, wawapeleke kwenye kundi lilelile. 6Wasipowaona wakamburura Yasoni na ndugu wengine, wakaenda nao kwa wakubwa wa mji wakipiga kelele na kusema: Watu hawa waliouchafua ulimwengu wamefika hata hapa,#Tume. 16:20. 7naye Yasoni ndiye aliyewafikiza. Hawa wote huyakanusha maagizo ya Kaisari wakisema: Mfalme ni mwingine, ni Yesu.#Luk. 23:2. 8Wakahangaisha watu wengi, hata wakubwa wa mji wakayasikia. 9Hao walipokwisha kumtoza Yasoni na wenzake mali zilizowatosha, wakawaacha, waende zao. 10Ndipo, ndugu walipomsindikiza Paulo na Sila papo hapo na usiku kwenda Beroya. Walipofika huko wakaingia nyumbani mwa kuombea mwa Wayuda. 11Hao walikuwa wema kuliko wale wa Tesalonike, wakalipokea Neno kwa mioyo iliyolipenda sana, kila siku wakayachunguza Maandiko, waone, kama ndivyo yalivyo kweli.#Yoh. 5:39. 12Hivyo wenzao wengi wakaja kumtegemea Bwana, vile vile hata kwa Wagriki wanawake na waume wenye cheo hawakuwa wachache. 13Lakini Wayuda wa Tesalonike walipotambua, ya kuwa Neno lake Mungu linatangazwa na Paulo hata huko Beroya, wakaja, wakawahangaisha watu nako huko.#1 Tes. 2:14. 14Papo hapo ndugu wakamsindikiza Paulo, wakamfikisha pwani. Lakini Sila na Timoteo wakakaa huko.#Tume. 16:1. 15Lakini wale waliomsindiza Paulo wakaenda naye mpaka Atene. Walipokwisha kupata maagizo ya kuwapelekea akina Sila na Timoteo, kwamba waje upesi sana kwake, wakaenda zao.
Kupiga mbiu mjini mwa Atene.
16*Paulo alipowangoja huko Atene akaumia rohoni mwake akiona, mji ulivyojaa miungu ya kutambikia. 17Akaongea nao Wayuda na watu wenye kumcha Mungu nyumbani mwa kuombea. Hata sokoni alisema kila siku na wale, aliowakuta hapo. 18Lakini kulikuwako wenye ujuzi wa chama cha Waepikurio na wa chama cha Wastoiko, wakabishana naye, wengine wakasema Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine tena wakasema: Anaonekana kuwa mtangazaji wa miungu migeni. Kwani alikuwa anawapigia hiyo mbiu njema ya Yesu na ya ufufuko.#1 Kor. 4:12. 19Ndipo, walipomshika, wakampeleka panapoitwa Areopago, wakamwuliza: Twaweza kutambua, yalivyo hayo mafundisho yako mapya, unayoyasema? 20Kwani unaingiza maneno mageni masikioni mwetu. Sasa twataka kutambua, hayo yatakapoelekea. 21Lakini wenyeji wote wa Atene na wageni waliotua humo hakuna, walichokitunukia kuliko kusema au kusikia yaliyo mapya.
22Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema: Enyi waume wa Atene, po pote ninawaona ninyi, mnavyotambikia miungu. 23Kwani nilipozunguka na kupatazama pa kuombea penu nikaona pa kuchinjia ng'ombe za tambiko palipoandikwa: Penye Mungu asiyetambulikana. Basi, huyo, mnayemtumikia pasipo kumjua, ndiye, ninayewatangazia. 24Mungu aliyeuumba ulimwengu navyo vyote vilivyomo hakai katika nyumba za kuombea zilizojengwa na mikono ya watu, kwani yeye ni Bwana wa mbingu na wa nchi.#Tume. 7:48. 25Naye hatumikiwi na mikono ya watu, tena hatumii kitu cho chote, kwani yeye mwenyewe ndiye aliyewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.#Sh. 50:12. 26Kwa tendo lake yeye watu wa mataifa yote wametoka kwa mmoja, wakakaa ko kote katika nchi zote zilizoko nchini; akawagawia huko kale siku zao za kuwapo, akawakatia nayo mipaka ya makao yao.#5 Mose 32:8. 27Alitaka, wamtafute Mungu, kama wanaweza kumnyatia, mpaka wamwone. Namo miongoni mwetu sisi hamna hata mmoja tu, ambaye anamkalia mbali.#Sh. 139; Yes. 55:6. 28Kwani yeye ndiye, tunayekalia, tunayeendea, tunayekuwa naye, kama watunga nyimbo walivyosema hata kwenu kwamba: Uzao wake ndio sisi. 29Basi, tukiwa uzao wake Mungu, haifai kumfananisha Mungu na maumbo ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe yaliyotengenezwa kwa uwezo na kwa mawazo ya kimtu.#1 Mose 1:27; Yes. 40:18-25. 30Siku za kujikalia tu na kupumbaa Mungu ameziacha tu, zipite; lakini sasa anawaagiza watu wote po pote, wajute.#Tume. 14:16; Luk. 24:47. 31Kwani ameweka siku, atakapompa mtu mmoja, aliyemwonea kazi hiyo, auhukumu ulimwengu wote kwa wongofu; lakini kwanza anawahimiza wote, wamtegemee, maana amemfufua katika wafu.#Tume. 10:42; Mat. 25:31; Rom. 10:14.
32Walipousikia ufufuko wa wafu, wengine wakamfyoza, wengine wakasema: Tunataka kukusikia na siku nyingine, utuelezee jambo hilo. 33Ndipo, Paulo alipotoka katikati yao. 34Lakini walikuwako waliogandamana naye, wakaja kumtegemea Bwana. Miongoni mwao alikuwamo mtu wa Areopago, ndiye Dionisio, tena mwanamke, jina lake Damari, na wengine waliokuwa pamoja nao.*

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 17: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

Video ya Matendo ya Mitume 17