Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 18

18
Paulo mjini mwa Korinto.
1Kisha Paulo akatoka Atene, akafika Korinto.#Rom. 16:3. 2Akaona Myuda mmoja, jina lake Akila, aliyezaliwa Ponto; naye alikuwa amekuja juzijuzi toka Italia pamoja na mkewe Puriskila, kwa sababu Kaisari Klaudio aliagiza, Wayuda wote watoke Roma. Akafikia kwao, 3kwa sababu kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi; maana walikuwa mafundi wa kushona mahema.#Tume. 20:34; 1 Kor. 4:12. 4Lakini kila siku ya mapumziko akabishana nao Wayuda na Wagriki nyumbani mwa kuombea, akawafundisha na kuwashinda.
5Lakini Sila na Timoteo walipofika toka nchi ya Makedonia, Paulo akafuliza kulitangaza Neno akiwashudia Wayuda, ya kuwa Yesu ndiye Kristo.#Tume. 17:14-15. 6Lakini walipopingamana naye na kumtukana, akawakung'utia mavumbi ya nguo zake, akawaambia: Damu zetu zitavijia vichwa vyenu! Mimi simo, ila nimetakata nikienda tangu sasa kwao wamizimu.#Tume. 13:46,51; 20:26. 7Akaondoka mle, akaingia nyumbani mwa mtu mwenye kumcha Mungu, jina lake Tiro Yusto, ambaye nyumba yake ilikuwa imepakana na nyumba ya kuombea. 8Lakini Krispo aliyekuwa mkubwa wa nyumba ya kuombea alimtegemea Bwana pamoja na waliokuwamo nyumbani mwake wote. Hata wenyeji wa Korinto wengi walipovisikia wakamtegemea, wakabatizwa.#1 Kor. 1:14. 9Bwana akamwambia Paulo kwa njozi usiku: Usiogope, tangaza tu, usinyamaze!#1 Kor. 2:3. 10Kwani mimi niko pamoja nawe, hakuna atakayekushika, akufanyie maovu. Kwani humu mjini ninao watu wengi.#Yer. 1:8; Hos. 2:23; Yoh. 10:16. 11Akakaa huko mwaka na miezi sita akifundisha kwao Neno la Mungu.
Galioni.
12Lakini Galioni alipokuwa bwana mkubwa wa nchi ya Akea, Wayuda wakapatana kumwunukia Paulo, wakampeleka bomani, 13wakasema: Huyu anawahimiza watu kumcha Mungu na kuyabeza Maonyo yake. 14Naye Paulo alipotaka kukifumbua kinywa chake, Galioni akawaambia Wayuda: Nyie Wayuda, mtu huyu kama amekosa kwa kufanya kibaya cho chote, ingalifaa kuwasikiliza vema.#Tume. 25:18-20. 15Lakini kama ni mabishano tu kwa ajili ya maneno na majina na maonyo ya kwenu, myatazame wenyewe! Mambo kama haya mimi sitaki kuyaamua.#Yoh. 18:31. 16Akawafukuza bomani.
17Ndipo, wote walipomkamata Sostene, mkubwa wa nyumba ya kuombea, wakampiga mbele ya boma; lakini nayo hayo Galioni hakuyatazama.
Kurudi Antiokia. Safari ya tatu ya Paulo.
18Paulo alipokwisha kukaa huko tena siku nyingi akaagana na ndugu, akatweka kwenda Ushami, Puriskila na Akila wakiwa pamoja naye; kwanza akanyoa kichwa kule Kenkerea, kwani alikuwa amejitia mwiko.#Tume. 21:24; 4 Mose 6:9,18. 19Walipofika Efeso, akawaacha huko; naye mwenyewe akaingia nyumbani mwa kuombea, akaongea na Wayuda. 20Lakini walipombembeleza, akae kwao kitambo, hakuwaitikia, 21ila akaagana nao akisema: Sikukuu itakayokuja sharti niimalizie Yerusalemu, lakini Mungu akitaka, nitarudi kwenu tena. Alipoondoka Efeso,#1 Kor. 4:19; Yak. 4:15. 22akatweka, akafika Kesaria, akapanda kuamkiana na wateule; kisha akatelemka kwenda Antiokia.#Tume. 21:15. 23Alipokwisha kukaa huko siku kidogo akaondoka tena, akakata nchi ya Galatia na ya Furigia na kuingia mji kwa mji akiwashupaza wanafunzi wote.
Apolo.
24Kulikuwa na Myuda, jina lake Apolo, aliyezaliwa Alekisandria; alikuwa na nguvu ya kusema, tena nguvu yake ilitoka katika utambuzi wa Maandiko; naye akafika Efeso.#1 Kor. 3:5-6. 25Huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana, akashurutishwa na Roho kusema na kuyafundisha mambo ya Yesu, yalivyo kweli, lakini aliujua ubatizo wa Yohana tu.#Tume. 19:3. 26Huyo alipoanza kutangaza nyumbani mwa kuombea waziwazi, Puriskila na Akila wakamsikia nao, wakampokea, wakamfunulia vema njia ya Mungu, aijue kabisa. 27Naye alipotaka kuvuka kwenda Akea, ndugu wakamtia moyo, wakawaandikia wanafunzi, wampokee. Alipofika huko akawasaidia sana waliogawiwa kumtegemea Bwana. 28Kwani aliwashinda sana Wayuda mbele za watu wote akionyesha na kuyaeleza Maandiko, ya kuwa Yesu ni Kristo.#Tume. 9:22; 17:3.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 18: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

Video ya Matendo ya Mitume 18