Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 10

10
Kornelio.
1Kesaria kulikuwa na mtu, jina lake Kornelio, mkubwa wa kikosi cha askari kilichoitwa cha Italia.#Mat. 8:5. 2Naye alimtii Mungu na kumcha pamoja nao wote wa nyumbani mwake: wengi wa kwao aliwagawia vipaji vingi, tena alikuwa akimwomba Mungu po pote. 3Siku moja, alipokuwa kama saa tisa ya mchana, akaona njozi, yuko macho, akaona, malaika wa Mungu akiingia nyumbani mwake na kumwambia: Kornelio! 4Naye akamkazia macho, akashikwa na woga, akasema: Nini, Bwana? Akamwambia: Maombo yako na magawio yako yamefika juu machoni pa Mungu, anayakumbuka. 5Sasa hivi tuma watu, waende Yope, wamlete Simoni anayeitwa Petero! 6amefikia kwa mtengenezaji wa ngozi, jina lake Simoni, nyumba yake iko pwani.#Tume. 9:43. 7Malaika aliyesema naye alipokwenda zake, akaita watumishi wawili na askari mwenye kumcha Mungu miongoni mwao walioshikana naye siku zote, 8akawasimulia yote, akawatuma, waende Yope.
Petero anatokewa na kitu.
9Kesho yake wale walipokuwa njiani na kuufikia mji karibu, Petero alikuwa amepanda kwenda katika chumba cha juu, aombe, saa sita ilipofika. 10Akaumwa na njaa, akataka kula. Walipomwandalia, akaingiwa na kituko, 11kwani anaona: mbingu imefunuka, kutoka mle panashuka chombo kinachofanana na guo kubwa, linatelemshwa chini, likishikwa kwa pembe zake nne.#Tume. 11:5-17. 12Mle ndani wamo nyama wote wenye miguu minne nao watambaao chini nao ndege wa angani. 13Kisha akasikia sauti ya kumwambia: Inuka, Petero, uchinje, ule! 14Ndipo, Petero aliposema: Hapana, Bwana! Kwani zamani zote sijala bado kilicho chenye mwiko au kisichotakata.#3 Mose 11; Ez. 4:14. 15Lakini sauti ikamwambia mara ya pili: Mungu alivyovitakasa, wewe usivizie!#Mat. 15:11. 16Vikafanyika hivyo mara tatu; kisha chombo kikapazwa mbinguni papo hapo.
17Petero alipopotelewa moyoni mwake, asijue maana ya hayo, aliyoyaona, papo hapo wale watu waliotumwa na Kornelio wakasimama mlangoni wakiiuliza nyumba ya Simoni. 18Wakapaza sauti na kuuliza, kama ndimo, Simoni anayeitwa Petero alimofikia. 19Naye Petero alipoyafikiri moyoni, aliyoyaona, Roho akamwambia: Tazama, pana watu watatu wanaokutafuta! 20Lakini inuka, ushuke, ufuatane nao pasipo mashaka! Kwani aliyewatuma ni mimi. 21Ndipo, Petero aliposhuka, akawajia wale watu, akawaambia: Tazameni, mnayemtafuta ni mimi. Mmekuja kwa sababu gani? 22Nao wakasema: Kornelio aliye mkubwa wa askari ni mtu mwongofu, mwenye kumcha Mungu, hata wote wa taifa la Wayuda wanamsemea vizuri; huyo ameagizwa na malaika mtakatifu, atume kwako, uje nyumbani mwake, ayasikie, utakayomwambia. 23Ndipo, alipowakaribisha na kuwafikiza.
Petero na Kornelio.
Kesho yake akainuka, akatoka pamoja nao, hata wengine wa Yope waliokuwa ndugu wakaenda pamoja naye. 24Siku ya kesho akaingia Kesaria. Naye Kornelio alikuwa akiwangoja; kwa hiyo alikuwa amewakusanya ndugu zake nao walio wapenzi wake wa kweli. 25Petero alipoingia, Kornelio akamwendea, akamwamkia na kumwangukia miguuni. 26Lakini Petero akamwinua akisema: Simama! kwani mimi nami ni mtu tu.#Tume. 14:15; Ufu. 19:10. 27Akaongea naye akiingia ndani; akawakuta wengi waliokusanyika, 28akawaambia: Ninyi mmejua, ya kuwa mtu wa Kiyuda ana mwiko wa kugandamiana na mtu wa kabila jingine au kumfikia. Lakini Mungu amenionyesha, nisimwazie mtu wo wote, kwamba ni wa mwiko au wa mzio. 29Kwa sababu hiyo nimekuja pasipo kubisha, ulipotuma kwangu. Sasa nawauliza: Ni neno gani, mlilonitumia? 30Kornelio akasema: Leo ni siku ya nne, tangu nilipokuwa nikifunga mpaka saa hii, tena nikimwomba Mungu nyumbani mwangu, saa tisa ilipofika. Papo hapo mtu alisimama mbele yangu aliyevaa nguo zilizomerimeta. 31Naye akasema: Kornelio, maombo yako yamesikiwa, nayo magawio yako yamekumbukwa mbele ya Mungu. 32Tume watu, waende Yope, wamwite Simoni anayeitwa Petero! Huyu amefikia nyumbani mwa Simoni aliye mtengenezaji wa ngozi, anakaa pwani. 33Papo hapo nikatuma kwako, nawe umefanya vema ukija. Sasa sisi sote tupo hapa mbele ya Mungu, tuyasikilize yote, uliyoagizwa na Bwana.
34*Petero akakifumbua kinywa chake, akasema: Naitambua kabisa iliyo kweli, ya kuwa Mungu hautazami uso wa mtu,#1 Sam. 16:7; Rom. 2:11. 35lakini katika mataifa yote anayemcha yeye na kufanya yaongokayo humpendeza.#Yoh. 10:16. 36Neno lake alilituma, liwafikie wana wa Isiraeli, akiwapigia ile mbiu njema ya utengemano uliopatikana kwa Yesu Kristo. Huyu ndiye Bwana wao wote.#Mat. 28:18. 37Ninyi mnayajua mambo yale yaliyofanyika katika nchi yote ya Yudea, yaliyoanza huko Galilea, Yohana alipokwisha kuutangaza ubatizo wake.#Mat. 4:12-17. 38Yesu wa Nasareti, Mungu alipomchagua kuwa mfalme na kumpa Roho takatifu na uwezo, alipita huko na huko akifanya mema na kuwaponya wote waliopagawa na yule Msengenyaji, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.#Yes. 61:1; Mat. 3:16; Yoh. 1:32. 39Nasi tumeyaona yote, aliyoyafanyiza katika nchi ya Wayuda namo Yerusalemu. Huyo walimwangamiza na kumtundika mtini, 40lakini Mungu akamfufua siku ya tatu, akamtuma, atokee;#1 Kor. 15:4-7. 41lakini sio watu wote waliotokewa naye, ni sisi tu tuliochaguliwa na Mungu kale, tuwe mashahidi; ni sisi tuliokula, tena tuliokunywa pamoja naye, alipokwisha kufufuka katika wafu.*#Yoh. 14:22; 15:27.
42*Akatuagiza kutangazia watu na kuyashuhudia po pote, ya kuwa ndiye aliyewekwa na Mungu, awahukumu wanaoishi nao waliokufa.#Tume. 17:31; Rom. 14:10; 1 Petr. 4:5. 43Kwa kumwelekea huyu Wafumbuaji wote hushuhudia, ya kuwa kila atakayemtegemea atapata kuondolewa makosa kwa Jina lake.#Yes. 53:5-6; Yer. 31:34; Ez. 34:16; Dan. 9:24.
44Petero akingali akiyasema maneno haya, Roho Mtakatifu akawaguia wote waliolisikia lile neno. 45Ndipo, wenye kumtegemea Bwana waliotahiriwa, waliokuja pamoja na Petero, waliposhangaa sana, ya kuwa hata wamaizimu humiminiwa kipaji cha Roho Mtakatifu. 46Kwani waliwasikia, wakisema misemo migeni na kumkuza Mungu. Ndipo, Petero alipojibu:#Tume. 2:4; Mar. 16:17. 47Yuko nani anayeweza kukataza maji, hawa wasibatizwe waliompokea Roho Mtakatifu sawasawa kama sisi? 48Akaagiza, wabatizwe katika Jina la Yesu Kristo.* Kisha wakamwomba, akae kwao siku kidogo.#Yoh. 4:40.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 10: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia