Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 9

9
1AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi. 2Akawatuma kuukhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3Akawaambia, Msichukue kitu cha njiani, fimbo wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala msiwe na kanzu mbili. 4Na nyumba yo yote mtakayoingia, kaeni humo, katokeni humo. 5Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao. 6Wakaenda zao, wakazunguka katika vijiji, wakiikhubiri injili, na kuponya watu killa pahali.
7Hatta Herode tetrarka akasikia yote yaliyotendwa nae, akaona mashaka, kwa kuwa wengine walisema kwamba Yohana amefufuka katika wafu: 8na wengine kwamba Eliya ametokea: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka. 9Herode akasema, Yohana nimemkata kichwa: bassi, nani huyu ambae ninasikia khabari zake za namna hii? Akatafuta kumwona.
10Wale mitume waliporudi wakamweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda zake kwa faragha mahali pasipo watu, karibu na mji uitwao Bethsaida. 11Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa. 12Hatta jua lilipoanza kuchwa wale thenashara wakamwendea wakamwambia, Uwaage makutano illi waende zao hatta vijiji vilivyo kandokando na mashamba wakapate mahali pa kulala na vyakula: maana hapa tulipo nyika tupu. 13Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki mbili, tusipokwenda sisi wenyewe tukawannnulie vyakula watu hawa wote. 14Kwa maana walikuwako wanaume wapata elfu tano. 15Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, killa safu watu khamsini. 16Wakafanya hivi, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi, kuviweka mbele ya makutano. 17Wakala, wakashiba wote: na vile vipande vilivyowabakia vikaokotwa, vikapu thenashara. 18Ikawra alipokuwa akisali peke yake wanafunzi wake walikuwa pamoja nae: akawanliza, akisema, Makutano huninena mimi kuwa nani? 19Wakajibu, wakasema, Yohana Mbatizaji: na wengine, Eliya: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka. 20Akawaambia, Na ninyi mwaninena mimi kuwa nani? 21Petro akajibu, akasema, Kristo wa Mungu. 22Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 23Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate. 24Kwa maana mtu akitaka kuisalimisha roho yake ataiangamiza, nae atakae kuitoa roho yake kwa ajili yangu, huyu ataisalimisha. 25Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote na kujipoteza, au kupata khasara ya roho yake? 26Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu. 27Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataionja mauti kabisa hatta watakapouona ufalme wa Mungu.
28Hatta baada ya maneno haya, panapo siku nane, akamchukua Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani kusali. 29Ikawa alipokuwa akisali, sura ya uso wake ikageuka, na mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta. 30Na tazama, watu wawili walikuwa wakisemezana nae, nao ni Musa na Eliya, 31walioonekana katika utukufu, wakanena khahari ya kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemi. 32Petro, nao waliokuwa pamoja nae, walikuwa wamelemewa sana na usingizi: lakini walipokwisha kuamka wakauona utukufu wake, na wale watu wawili, waliosimama pamoja nae. 33Ikawa hawo walipokuwa wakijitenga nae, Petro akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, kimoja cha Eliya: nae hajui asemalo. 34Hatta alipokuwa akisema haya likawako wingu, likawatia uvuli; wakaogopa walipoingia katika lile wingu. 35Sauti ikatoka katika lile wingu ikasema, Huyu ni Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 36Na sauti hii ilipokuja Yesu akaonekana peke yake. Nao wakanyamaza wasimwambie mtu siku zile neno lo lote la hayo waliyoyaona.
37Ikawa siku ya pili yake, waliposhuka mlimani, mkutano mkuu wakakutana nae. 38Na tazama, mtu mmoja katika ule mkutano akapaaza sauti yake, akisema, Mwalimu, nakuomha, mwangalie mwanangu, kwa kuwa yeye ni mwanangu pekee; 39na tazama, pepo humshika, nae marra hulia; tena humrarua, akatoka povu, wala hamtoki illa kwa shidda, akimchubuachubua. 40Nikawaomba wanafunzi wako wamfukuze, wasiweze. 41Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisichoamini na upofu, nikae nanyi hatta hui? Mlete mwana wako hapa. 42Alipokuwa katika kumwendea, yule pepo akambwaga akamraruararua. Yesu akamkaripia yule pepo mchafu, akamponya yule mtoto, akamrudishia baba yake. 43Watu wote wakashangaa kwa adhama yake Mungu.
Hatta wote walipokuwa wakistaajabia mambo yote aliyoyafanya akawaambia wanafunzi wake, 44Yawekeni maneno haya masikioni mwenu: kwa maana Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu. 45Lakini hawakulifuhamu neno lile, likawa limefichwa kwao wasipate kulitambua. Wakaogopa kumwuliza maana ya neno lile. 46Yakawaingia mabishano, ni nani atakaekuwa mkubwa miongoni mwao. 47Nae Yesu alipoona mawazo ya mioyo yao, akatwaa kitoto akamweka karibu yake, 48akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.
49Yohana akajibu, akasema, Mwalimu, tulimwona mtu anafukuza pepo kwa jina lako, tukamkataza kwa kuwa hatufuati sisi. 50Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa maana yeye asiye kinyume chetu ni upande wetu. 51Ikawa siku za kupandishwa kwake juu zilipokuwa karibu kutimia, yeye mwenyewe akauelekeza nso wake kwenda Yerusalemi. 52Akatuma wajumbe mbele ya uso wake, wakashika njia, wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, illi kumfanyia tayari. 53Nao hawakumkaribisha, kwa sababu nso wake ameuelekeza kwenda Yerusalemi. 54Wanafunzi wake Yokobo na Yohana walipoona haya, wakasema, Bwana, wataka tuambie moto ushuke kutoka mbinguni uwaangamize, kama na Eliya alivyofanya? 55Akageuka, akawakaripia, akasema, Hamjui ni moyo wa namna gani mlio nao. 56Maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za wana Adamu, bali kuziokoa. Wakaenda zao hatta mji mwingine.
57Na walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja akamwambia, Nitakufuata ko kote uendako, Bwana. 58Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vioto vyao, bali Mwana wa? Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. 59Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe rukhusa niende kwanza, nikamzike baba yangu. 60Akamwambia, Waache wafu wazike wafu wao, bali wewe enenda zako ukautangaze ufalme wa Mungu. 61Na mwingine nae akasema, Nitakufuata, Bwana, lakini kwanza nipe rukhusa nikawaage watu wa nyumbani mwangu. 62Yesu akamwambia, Hakuna mtu aliyetia mkono wake alime, khalafu akatazama nyuma, afaae kwa ufalme wa Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 9: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia