Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 10

10
1BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe. 2Akawaambia, Mavuno ni mengi, illakini watenda kazi wachache; mwombeni, bassi, Bwana wa mavuno, apate kupeleka watenda kazi mavunoni mwake. 3Enendeni: angalieni, nakutumeni ninyi kama wana kondoo kati ya mbwa wa mwitu. 4Msichukue kifuko, wala mkoba, wala viatu: wala msimsalimu mtu njiani. 5Na nyumba yo yote mwingiayo, kwanza neneni, Amani iwe nyumbani humu. 6Na kama yumo mwana wa amani, amani yenu itakaa kwake. La! si hivyo, itawarudia ninyi. 7Kaeni katika nyumba hiyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; kwa maana mtenda kazi astahili kupewa ijara yake.
8Msihame nyumba kwa nyumba. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisheni, vileni vitu vile viwekwavyo mbele yenu. 9Waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni ya kama, Ufalme wa Mungu umewakaribieni. 10Na mji wo wote mtakaouingia nao hawawakaribishi utokeni, mkipita katika njia zake semeni, 11Hatta mavumbi haya ya mji wenu, yaliyogandamana nasi, twayakungʼuta juu yenu: illakini jueni haya, ya kuwa ufalme wa Mungu umewakaribieni. 12Nawaambieni, itakuwa rakhisi Sodoma istahimili adhabu yake siku ile kuliko mji ule. 13Ole wako, Korazin! Ole wako Bethsaida! kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingalifanyika katika Turo na Sodom, wangalitubu zamani, wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. 14Lakini itakuwa rakhisi Turo na Sidoni istahimili adhabu zao siku ile ya hukumu, kuliko ninyi. 15Nawe Kapernaum, wewe uliyeinuliwa hatta mhinguni, ntashushwa hatta kuzimu. 16Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.
17Wale sabaini wakarudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hatta pepo wanatutii kwa jina lako. 18Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni. 19Tazameni, nawapeni mamlaka va kuwakanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hapana kitu kitakachowadhuru ninyi kamwe. 20Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.
21Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako. 22Akawagenkia wanafunzi wake akasema, Nimekahidhiwa vyote na Baba yangu: wala hapana mtu ajuae khabari za Mwana illa Baba: wala khabari za Baha illa Mwana, na mtu ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia. 23Akawageukia wanafunzi wake kwa faragha, akawaambia, Ya kheri macho yatazamayo mnayoyatazama ninyi. 24Maana nawaambia; Manabii wengi na wafalme walitaka kuyaona mnayoyatazama ninyi wasiyaone, na kuyasikia mnayoyasikia wasiyasikie.
25Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele? 26Akamwambia, Katika torati imeandikwa nini? Wasomaje? 27Nae akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. 28Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi, ndipo utaishi. 29Nae akitaka kujifanya ana haki akamwambia Yesu, Na jirani yangu ni nani? 30Yesu akajibu akasema, Kulikuwa na mtu akishuka kutoka Yerusalemi kwenda Yeriko; akaangukia katika mikono ya wanyangʼanyi, wakamvua nguo zake, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakamwacha nussu ya kufa. 31Na kwa nasibu kukashuka kuhani mmoja njia ileile, akamwona, akapita upande. 32Na Mlawi kadhalika alipofika pahali pale, akamwona akapita upande. 33Lakini Msamaria mmoja akisafiri, akamjia, nae alipomwona akamhurumia; 34bassi akamjongelea, akamfunga jeraha zake, akitia mafuta na mvinyo: akampandisha juu ya nyama wake, akamleta katika nyumba ya wageni, akamwuguza. 35Hatta assubuhi yake akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba, akasema, Mwuguze: na cho chote utakachogharimia zaidi, nirudipo, nitakulipa. 36Waonaje bassi? Katika hawa watatu yupi aliyekuwa jirani yake mwenye kuangukia katika mikono ya wanyangʼanyi? 37Akasema, Ni yule aliyemfanyia huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye kama hayo.
38Nao walipokuwa wakienenda, akaingia katika kijiji kimoja; na mwanamke mmoja, jina lake Martha, akamkaribisha nyumbani mwake. 39Nae alikuwa na ndugu mwanamke aitwae Mariamu, nae alikuwa ameketi miguuni pa Yesu, akasikia maneno yake. 40Bali Martha alihangaika kwa khuduma nyingi: akamwendea, akasema, Bwana, haikukhussu wewe ya kuwa ndugu yangu ameniacha kukhudumu peke yangu? Bassi mwambie anisaidie. 41Bwana akamjibu akamwambia, Martha, Martha, unajisumbua na kujifadhaisha kwa ajili ya mambo mengi: 42lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu ameichagua sehemu iliyo njema, ambayo hataondolewa.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 10: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia