Luka MT. 6
6
1IKAWA siku ya Sabato alikuwa akipita katika makonde, wanafunzi wake wakavunja masuke, wakayala, wakiyapukusapukusa mikononi mwao. 2Bassi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnatenda lisilo halali siku ya Sabato? 3Yesu akajibu, akawaambia, Hatta neno hili hamkulisoma, alilolitenda Daud, alipokuwa na njaa, yeye nao waliokuwa pamoja nae, 4jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate iliyotolewa kwa Mungu, akaila, akawapa na hawo waliokuwa pamoja nae, isiyo halali kuliwa illa na makuhani peke yao? 5Akawaambia ya kwamba, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia.
6Ikawa Sabato nyingine akaingia katika sunagogi, akafundislia: na palikuwako huko mtu mwenye mkono umepooza, mkono wa kuume. 7Mafarisavo na waandishi wakamvizia kuona kwamba ataponya siku ya Sabato, wapate kumshitaki. 8Lakini yeye akatambua mawazo yao, akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Ondoka, kasimama katikati. 9Yesu akawaambia, Nitawaulizeni neno moja. Ni halali siku ya Sabato kutenda mema au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? 10Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. 11Akatenda hivyo. Mkono wake ukapona, ukawa mzima kama wa pili. Nao wakatekewa moyo: wakisemezana wao kwa wao, wamtendeje Yesu.
12Ikawa katika siku zile akaomloka akaenda mlimani kuomba, akashinda usiku kucha, akimwomba Mungu. 13Ulipokuwa mchana akawaita wanafunzi wake: akachagua watu thenashara miongoni mwao, ambao aliwaita mitume. 14Simon ambae alimpa jina la pili Petro, na Andrea, ndugu yake; Yakobo na Yohana, Filipo na Bartholomayo. 15Mattayo na Tomaso, Yakobo wa Alfayo, na Simon aliyeitwa Zelote, 16Yuda wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa khaini. 17Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao; 18nao waliosumbuliwa na pepo wachafu; wakaponywa. 19Makutano yote wakatafuta kumgusa: kwa maana nguvu zilikuwa zikimtoka, zikawaponya wote.
20Nae akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, M kheri ninyi mlio maskini: kwa sababu ufalme wa Mungu ni wemi. 21M kheri ninyi mnaoona njaa sasa: kwa subabu mtashiba. M kheri ninyi mliao sasa: kwa sababu mtacheka. 22M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu. 23Furahini siku ile, mkaruke: kwa kuwa bakika thawabu yenu nyiugi mbinguni, maana baba zao waliwatenda manabii mambo kama hayo. 24Bali ole wemi ninyi mlio na mali: kwa sababu mmekwisha kuwa na faraja yenu. 25Ole wenu ninyi mlioshiba: kwa sababu mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa: kwa sababu mtaomboleza na kulia. 26Ole wenu ninyi, wana Adamu wote watakapowanena vema: maana baba zao waliwatenda manabii ya uwongo mambo kamsi hayo.
27Bali nawaambia ninyi mnaosikiliza, Wapendeni adui zenu, watendeni mema wao wawachukiao ninyi, 28wabarikini wao wawalaanio ninyi, waombeeni wao watendao ninyi jeuri. 29Akupigae shavu moja, umgeuzie la pili, nae akunyangʼanyae joho yako usimzuilie na kanzu. 30Killa akuombae mpe; nae akunyangʼanyae mali zako, usitake akurudishie. 31Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, nanyi watendeeni vivyo hivyo. 32Bassi mkiwajienda wao wawapendao ninyi mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi huwapenda wao wawapendao. 33Na mkiwatenda mema wao wawatendao ninyi mema, mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. 34Na mkikopesha watu mkitumaini kupata kitu kwao tena, mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi hukopesha wenye dhambi, illi wapokee sawasawa. 35Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.
36Bassi mwe na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa: 37msipatilize, nanyi hamtapatilizwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. 38Toeni, nanyi mtapewa: kipimo chema kilichoshindiliwa, kilichosukwasukwa, kinachofurika ndicho watu watakachowapa ninyi kifuani mwenu. Kwa maana kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa na ninyi. 39Akawaambia mfano, Aweza kipofu kumwongoza kipofu? Hawatatumbukia wote wawili shimoni? 40Mwanafunzi hampiti mwalimu wake; illa killa aliyekhitimu atakuwa sawa na mwalimu wake. 41Bassi, mbona watazama kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, na boriti iliyomo jichoni mwako huioni? 42Au wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, niache niondoe kibanzi kilichomo jichoni mwako, na wewe mwenyewe huioni boriti iliyomo jichoni mwako? Mnafiki, toa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako, ndipo utakapoona vema kutoa kibanzi jichoni mwa ndugu yako.
43Maana hapana mti mwema uzaao matunda mabovu; wala mti mbovu uzaao matunda mema. 44Kwa maana killa mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa kuwa katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. 45Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa lililo jema: na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa lililo ovu: kwa sababu kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 46Ya nini kuniita Bwana, Bwana, nanyi hamyatendi niyanenayo? 47Killa mtu ajae kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda nitawaonyesha mfano wake mtu huyu. 48Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba. 49Nae asikiae bila kutenda afanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo pasipo msingi: bassi mto ukairukia kwa nguvu, ikaanguka marra, na kuanguka kwake ile nyumba kulikuwa kukubwa.
Iliyochaguliwa sasa
Luka MT. 6: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.