Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 5

5
1IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti: 2akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa: na wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. 3Akaingia chombo kimoja, kilichokuwa cha Simon, akamtaka asogeze kidogo kutoka pwani. Akakaa, akawafundisha makutano katika chombo. 4Alipokwisha kusema, akamwambia Simon, Sogea hatta kilindini, mkashushe nyavu zenu kwa uvuvi. 5Simon akajibu, akasema, Bwana, tulisumbuka usiku kucha, tusipate kitu: illakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 6Bassi, walipofanya hivi, wakakusanya wingi wa samaki: nyavu zao zikaanza kukatika. 7Wakawaashiri wenzi wao katika chombo cha pili, waje kuwasaidia. Wakaenda wakavijaza vyombo vyote viwili, hatta kuvizamisha. 8Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. 9Kwa maana ushangao umemshika yeye, na wote waliokuwako pamoja nae, kwa uvuvi wa samaki walioupata. 10Kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washiriki wa Simon, Yesu akamwambia Simon, Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu. 11Na walipoleta vyombo pwani, wakaacha vyote wakamfuata.
12Ikawa alipokuwa katika mji mmoja wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejawa ukoma; nae alipomwona Yesu, akaanguka kifudifudi, akamwomba, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 13Nae akauyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka; takasika. Marra ukoma wake ukamwounoka. 14Akamwagiza asimwambie mtu: illa enenda, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe kwa kutakasika kwako alivyoamuru Musa, illi kuwa ushuhuda kwao. 15Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. 16Lakini yeye alikuwa akijitenga jangwani na kusali.
17Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya. 18Na kumbe! watu wanachukua mtu kitandani mwenye kupooza: wakitaka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. 19Hatta walipokosa pa kumpeleka ndani kwa sababu ya lile kundi la watu, wakapanda juu ya dari wakampisha katika matofali, wakamshusha na kitanda chake hatta katikati mbele ya Yesu. 20Alipoona imani yao, akamwambia, Ee mtu, dhambi zako zimeondolewa. 21Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu? 22Yesu akafahamu fikara zao akajibu, akawaambia, Mnafikiri nini mioyoni mwenu? 23Vipi vyepesi, kusema, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, ukaende. 24Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dhambi (alimwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako. 25Marra akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, akimhimidi Mungu. 26Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo.
27Baada ya haya akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, amekaa forodhani, akamwambia, Nifuate. 28Akaacha vyote akaondoka akamfuata. 29Nae Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake: na palikuwa na kundi kubwa la watoza ushuru, na watu wengine waliokuwa wameketi pamoja nao chakulani. 30Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 31Yesu akajibu, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi: 32sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu. 33Nao wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana wanafunga marra nyingi na kusali, na wanafunzi wa Mafarisayo wanafanya vilevile, bali wanafunzi wako hula na hunywa? 34Yesu akawaambia, Je! mwaweza kuwafungislia wana wa arusi, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? 35Lakini siku zitakuja watakapoondolewa Bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile. 36Akawaambia mithali, Hakima apasuae kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu: ikiwa atia aipasua ile mpya, na kile kiraka cha nguo mpya hakilingani na lile vazi kuukuu. 37Wala hakuna mtu atiae divai mpya katika viriba vikuukuu: ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe ikamwagika, viriba vikapotea. 38Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya. 39Wala hakuna mtu anywae divai ya kale, marra akatamani divai mpya, maana asema, Ile ya kale ni njema zaidi.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 5: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia