Luka MT. 7
7
1ALIPOKWISHA kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu akaingia Kapernaum.
2Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana. 3Aliposikia khabari za Yesu akatuma baadhi ya wazee wa Wayahudi kwake, akimwomba aje, amwokoe mtumishi wake. 4Nao walipolika kwa Yesu, wakamsihi kwa jubudi wakisema, 5ya kama, Astahili umtendee neno hili, maana apenda taifu letu, nae alitujengea sunagogi letu. 6Bassi Yesu akaenda pamoja nao. Hatta alipokuwa si mbali ya nyumba yake, yule akida akatuma rafiki kwake akimwambia, Bwana, usijisumbue, 7maana si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: kwa biyo nalijiona sistahili kuja kwako: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 8Sababu mimi nami ni mtu aliyewekwa chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda: na huyu, Njoo, huja; na mtumishi wangu, Fanya hivi, hufanya. 9Yesu aliposikia haya akamstaajabia akawageukia makutano waliokuwa wakimfuata, akisema, Nawaambieni, Hatta katika Israeli sikuona imani nyingi namna hii. 10Bassi wale waliotumwa waliporudi nyumbani kwake, wakamkuta yule mtumishi, aliyekuwa hawezi, yu mzima.
11Ikawa khalafu yake, akaenda mji uitwao Nain, wanafunzi wake na watu wengi wakafuatana nae. 12Bassi, alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, mwana pekee wa mama yake, nae mjane; na watu wa mji wengi pamoja nae. 13Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie. 14Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka. 15Yule maiti akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake. 17Zikatoka hizo khabari zake katika Yahudi yote, na katika inchi yote iliyozunguka.
18Bassi wanafunzi wake Yohana wakamwarifu haya yofe. 19Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine? 20Bassi watu hawo walipofika kwake wakasema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiye ajae au tumtazamie mwingine? 21Saa ileile akawaponya watu wengi maradhi zao, na misiba yao, na pepo wabaya: na vipofu wengi akawakarimia kuona. 22Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema: 23na yu kheri ye yote asiyechukizwa nami.
24Na wale wajumbe wa Yohana, walipokwisha kwenda zao, akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 25Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Fahamuni, watu wenye nguo za umalidadi na kuishi maisha ya anasa wamo katika majumba ya wafalme. 26Bali mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambieni, na aliye zaidi ya nabii. 27Huyu ndiye aliyeandikiwa, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakaeitengeneza njia yako mbele yako. 28Maana nawaambieni, Katika wazao wa wanawake hapana nabii aliye mkuu kuliko Yobana Mbatizaji: lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye. 29Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae. 31Bwana akasema, Nitawafananisha na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? 32Wamefanana na watoto, waketio sokoni, wakiitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi nanyi hamkucheza, tuliomboleza, nanyi hamkulia. 33Kwa maana Yohana Mbatizaji amekuja, hali mkate, wala hanywi divai, mkasema, Yuna pepo. 34Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi. 35Na hekima imepata haki yake kwa watoto wake wote.
36Mtu mmoja katika Mafarisayo akamtaka ale chakula pamoja nae. Akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37Kumbe! Mwanamke mmoja katika mji ule ahyekuwa mwenye dhambi, alipopata khabari ya kuwa ameketi katika nyumba ya yule Farisayo, akaleta chupa cha alabastro yenye marhamu, 38akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumchuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake akibusu sana miguu yake, na kuipaka yale marhamu. 39Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. 40Yesu akajibu akamwambia, Simon, nina neno la kukuambia. Akanena, Mwalimu, sema. 41Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili: mmoja aliwiwa nae dinari khamsi mia, na wa pili khamsini. 42Nao wakiwa hawana kitu cha kulipa, akawasamehe wote wawili. Bassi, sema, Katika hawo ni nani atakaempenda zaidi? 43Simon akajibu akasema, Nadhani ni yule aliyesamehewa nae mengi. Akamwambia, Umehukumu haki. 44Akamgenkia yule mwanamke, akamwambia Simon, Wamwona mwanamke huyu? Naliingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawia miguu, bali huyu amenichuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. 45Hukunibusu: bali huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu. 46Hukunipaka kichwa changu mafuta: bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. 47Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo. 48Akamwambia, Umesamehewa dhambi zako. 49Na wale walioketi pamoja nae wakaanza kusema ndani ya mioyo yao, Nani huyu hatta akasamehe dhambi? 50Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa; enenda zako kwa amani.
Iliyochaguliwa sasa
Luka MT. 7: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.