Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 4

4
Maono ya tano: Kinara cha taa na miti ya mizeituni
1 # Dan 8:18 Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake. 2#Kut 25:31,37; Ufu 4:5 Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake; 3#Ufu 11:4 na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kulia wa lile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. 4Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini? 5Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. 6#Ezr 5:2 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi. 7#Isa 40:3,4; Mt 21:21; Zab 118:22; Ezr 3:11 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie. 8Tena neno la BWANA likanijia, kusema, 9#Ezr 6:15; 1 Kor 2:4 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. 10#Hag 2:3; 2 Nya 16:9; Ufu 5:6 Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa#4:10 Katika Kiebrania hakuna taa. saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote. 11#Ufu 11:4 Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kulia wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto? 12Na kwa mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao? 13Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. 14#1 Sam 2:10 Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili watiwa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.

Iliyochaguliwa sasa

Zekaria 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha