Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 5

5
Maono ya sita: Gombo linalopuruka
1Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la kitabu lirukalo. 2Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la kitabu lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi. 3#Mit 3:33; Isa 24:6; Mal 4:6; Gal 3:10,13; Ebr 6:8 Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atakatiwa mbali kama ilivyoandikwa upande, na kwa hiyo kila aapaye kwa uongo#5:3 Maneno ‘kwa uongo’ yameongezwa kutoka kwa mstari wa 4. atakatiliwa mbali kama ilivyo andikwa upande wa pili. 4#Law 19:12; 14:45; Mt 5:33-36; Yak 5:12 Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.
Maono ya saba: Mwanamke akiwa katika kikapu
5Ndipo yule malaika aliyesema nami akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho. 6Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote; 7na tazama, kifuniko#5:7 Katika Kiebrania ni ‘talanta’. cha risasi kiliinuliwa; na tazama, mlikuwa na mwanamke ndani ya kikapu. 8Akasema, Huyu ni Uovu; akamsukuma ndani ya kile kikapu; akalitupa lile jiwe la risasi juu ya mdomo wa ile efa. 9Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu. 10Ndipo nikamwambia yule malaika aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii? 11#Yer 29:5 Akaniambia, Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari;#5:11 Ni jina la zamani la Babeli. tena ikiisha kutengenezwa, atawekwa huko mahali pake mwenyewe.

Iliyochaguliwa sasa

Zekaria 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia