Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 3

3
Maono ya nne: Yoshua na Shetani
1 # Hag 1:1; Ayu 1:6; Ezr 5:2; Ufu 12:10 Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kulia ili kushindana naye. 2#Zab 109:31; Mt 4:10; Lk 22:31; Yud 1:9; Rum 16:20; 8:33; 11:5 BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je, Hiki si kinga kilichotolewa motoni? 3#Isa 64:6 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika. 4#Ufu 19:8 Naye malaika akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi chafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani kubwa. 5#Kut 29:6 Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa BWANA akasimama karibu. 6Kisha malaika wa BWANA akamshuhudia Yoshua, akisema, 7#Kum 17:9 BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
8 # Isa 42:1; 4:2; Yer 23:5; 33:15; Zek 6:12 Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako wanaoketi mbele yako; maana hao ni watu walio ishara ya mambo yajayo; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi. 9#Isa 28:16; 53:4; Ufu 5:6 Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja ziko nyuso saba; tazama, nitachonga maandishi yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi hii katika siku moja. 10#1 Fal 4:25; Mik 4:4 Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ninyi mtamwalika kila mtu jirani yake chini ya mzabibu, na chini ya mtini.

Iliyochaguliwa sasa

Zekaria 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia