Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 9:1-10

Zaburi 9:1-10 SRUV

Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Nitafurahi na kukushangilia; Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu. Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako. Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki. Umewakemea mataifa; Na kumwangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele; Adui wameangamia na kuwa magofu milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea. Bali BWANA atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu. Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa uadilifu. BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida. Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

Soma Zaburi 9

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 9:1-10

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha