Zab 9:1-10
![Zab 9:1-10 - Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote;
Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;
Nitafurahi na kukushangilia Wewe;
Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu.
Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma;
Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
Kwa maana umenifanyia hukumu na haki
Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.
Umewakemea mataifa;
Na kumwangamiza mdhalimu;
Umelifuta jina lao milele na milele;
Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele.
Nayo miji yao uliing’oa;
Hata kumbukumbu lao limepotea.
Bali BWANA atakaa milele,
Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki;
Atawaamua watu kwa adili.
BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa,
Naam, ngome kwa nyakati za shida.
Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,
Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F320x320%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fstatic-youversionapi-com%2Fimages%2Fbase%2F26196%2F1280x1280.jpg&w=640&q=75)
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu. Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako. Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki. Umewakemea mataifa; Na kumwangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele; Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele. Nayo miji yao uliing’oa; Hata kumbukumbu lao limepotea. Bali BWANA atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu. Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa adili. BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida. Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.
Zab 9:1-10