Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 59:1-9

Zaburi 59:1-9 SRUV

Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami. Uniponye nao wafanyao maovu, Uniokoe na watu wa damu. Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu. Bila kosa langu wanaenda mbio, kujiweka tayari; Inuka utazame na kunisaidia. Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uinuke. Uwapatilize mataifa yote; Usimrehemu hata mmoja wa wale wapangao maovu kwa hila. Wakati wa jioni hurudi, wakilia kama mbwa, Na kuzungukazunguka mjini. Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye? Na Wewe, BWANA, utawacheka, Utawadhihaki mataifa yote. Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu.

Soma Zaburi 59