Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 22:22-30

Zaburi 22:22-30 SRUV

Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu. Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wazawa wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazawa wa Israeli. Maana hapuuzi Wala kuchukizwa na mateso ya anayeteswa, Wala hamfichi uso wake, Bali humsikia akimlilia. Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao. Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao BWANA watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele. Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia. Maana ufalme ni wa BWANA, Naye ndiye awatawalaye mataifa. Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake, Wazawa wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za BWANA, Kwa kizazi kitakachokuja

Soma Zaburi 22

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 22:22-30

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha