Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 22:22-30

Zaburi 22:22-30 NEN

Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. Ninyi ambao mnamcha BWANA, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe. Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao BWANA watamsifu: mioyo yenu na iishi milele! Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia BWANA, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake, kwa maana ufalme ni wa BWANA naye hutawala juu ya mataifa. Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. Wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao. Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 22:22-30

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha