Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 22:22-30

Zab 22:22-30 SUV

Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu. Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli. Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia. Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao. Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao BWANA watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele. Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia. Maana ufalme una BWANA, Naye ndiye awatawalaye mataifa. Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake, Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za BWANA, Kwa kizazi kitakachokuja

Soma Zab 22

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 22:22-30

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha