Zaburi 148:7-10
Zaburi 148:7-10 SRUV
Msifuni BWANA kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote. Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba utimizao neno lake. Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote. Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.