Zaburi 148:7-10
Zaburi 148:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Msifuni BWANA kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote. Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake. Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote. Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
Zaburi 148:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Msifuni Mwenyezi-Mungu kutoka duniani; enyi majoka ya baharini na vilindini, msifuni. Msifuni enyi moto, mvua ya mawe na theluji, upepo wa tufani unaotimiza amri yake! Msifuni enyi milima na vilima, miti ya matunda na misitu! Msifuni enyi wanyama wa porini na wafugwao, viumbe vitambaavyo na ndege wote!
Zaburi 148:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Msifuni BWANA kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote. Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba utimizao neno lake. Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote. Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
Zaburi 148:7-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mtukuzeni BWANA kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari, umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote, wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao