Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 147:10-20

Zaburi 147:10-20 SRUV

Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji. BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake. Msifu BWANA, Ee Yerusalemu; Msifu Mungu wako, Ee Sayuni. Maana amevikaza vipingo vya malango yako, Amewabariki wanao ndani yako. Ndiye aletaye amani mipakani mwako, Hukushibisha kwa ngano safi. Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana. Ndiye atoaye theluji kama sufu, Huimwaga barafu yake kama majivu, Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama? Hulituma neno lake na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka. Hulitangaza neno lake kwa Yakobo, Na amri zake na hukumu zake kwa Israeli. Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya.

Soma Zaburi 147