Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 147:10-20

Zaburi 147:10-20 NEN

Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu. BWANA hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma. Mtukuze BWANA, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni, kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako. Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa. Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi. Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu. Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake? Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka. Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake.