Zaburi 147:10-20
Zaburi 147:10-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari; lakini hupendezwa na watu wamchao, watu wanaotegemea fadhili zake. Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee Yerusalemu! Umsifu Mungu wako, ee Siyoni! Maana yeye huimarisha milango yako, huwabariki watu waliomo ndani yako. Huweka amani mipakani mwako; hukushibisha kwa ngano safi kabisa. Yeye hupeleka amri yake duniani, na neno lake hufikia lengo lake haraka. Hutandaza theluji kama pamba, hutawanya umande kama majivu. Huleta mvua ya mawe kama kokoto na kwa ubaridi wake maji huganda. Kisha hutoa amri, maji hayo yakayeyuka; huvumisha upepo wake, nayo yakatiririka. Humjulisha Yakobo ujumbe wake, na Israeli masharti na maagizo yake. Lakini hakuyatendea hivyo mataifa mengine; watu wengine hawayajui maagizo yake. Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Zaburi 147:10-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mtu. BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake. Msifu BWANA, Ee Yerusalemu; Msifu Mungu wako, Ee Sayuni. Maana ameyakaza mapingo ya malango yako, Amewabariki wanao ndani yako. Ndiye afanyaye amani mipakani mwako, Akushibishaye kwa unono wa ngano. Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana. Ndiye atoaye theluji kama sufu, Huimwaga barafu yake kama majivu, Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama? Hulituma neno lake na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka. Humhubiri Yakobo neno lake, Na Israeli amri zake na hukumu zake. Hakulitendea taifa lo lote mambo kama hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya.
Zaburi 147:10-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu. BWANA hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma. Mtukuze BWANA, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni, kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako. Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa. Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi. Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu. Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake? Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka. Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake.
Zaburi 147:10-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji. BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake. Msifu BWANA, Ee Yerusalemu; Msifu Mungu wako, Ee Sayuni. Maana amevikaza vipingo vya malango yako, Amewabariki wanao ndani yako. Ndiye aletaye amani mipakani mwako, Hukushibisha kwa ngano safi. Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana. Ndiye atoaye theluji kama sufu, Huimwaga barafu yake kama majivu, Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama? Hulituma neno lake na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka. Hulitangaza neno lake kwa Yakobo, Na amri zake na hukumu zake kwa Israeli. Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya.