Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 136

136
Uumbaji wa Mungu na matukio ya kihistoria
1 # 1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 118:1; Yer 33:11 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 # Kut 18:11; Kum 10:17 Mshukuruni Mungu wa miungu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3 # 1 Tim 6:15; Ufu 17:14 Mshukuruni Bwana wa mabwana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4Yeye peke yake afanya maajabu makuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5 # Mwa 1:1; Mit 3:19 Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6 # Mwa 1:2; Yer 10:12 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7 # Mwa 1:16; Kum 4:19 Yeye aliyeumba mianga mikubwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8Jua litawale mchana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9Mwezi na nyota zitawale usiku;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10 # Kut 12:29 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11 # Kut 12:51 Akawatoa Waisraeli katikati yao;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13 # Zab 78:13; Kut 14:21-29 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14Akawavusha Israeli katikati yake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16 # Kum 8:15 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18 # Kum 29:7 Akawaua wafalme mashuhuri;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19 # Hes 21:21-30 Sihoni, mfalme wa Waamori;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20 # Hes 21:31-35 Na Ogu, mfalme wa Bashani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21 # Yos 12:1 Akaitoa nchi yao iwe urithi;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22Urithi wa Israeli mtumishi wake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23 # Mwa 8:1; Kum 32:36; Zab 102:17; Isa 63:9; Lk 1:48 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24Akatuokoa na watesi wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25 # Zab 104:27 Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26Mshukuruni Mungu wa mbingu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 136: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia