Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 135

135
Sifa kwa wema na ukuu wa Mungu
1Haleluya.
Lisifuni jina la BWANA,
Enyi watumishi wa BWANA, sifuni.
2 # Lk 2:37 Ninyi msimamao nyumbani mwa BWANA,
Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu.
3Msifuni BWANA kwa kuwa BWANA ni mwema,
Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.
4 # Kut 19:5; Kum 7:6,7 Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo,
Na Israeli, wawe watu wake hasa.
5Maana najua ya kuwa BWANA ni mkuu,
Na Bwana wetu yuko juu ya miungu yote.
6BWANA amefanya kila lililompendeza,
Katika mbingu na katika nchi,
Katika bahari na katika vilindi vyote.
7 # Mwa 2:6; Ayu 5:10; Yer 10:13; Zek 10:1; Ayu 28:25; 38:22 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi;
Huifanyia mvua umeme;
Hutoa upepo katika ghala zake.
8Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri,
Wa wanadamu na wa wanyama.
9Alituma ishara na maajabu kati yako, Ee Misri,
Juu ya Farao na watumishi wake wote.
10 # Hes 21:24 Aliwapiga mataifa mengi,
Akawaua wafalme wenye nguvu;
11 # Yos 12:7 Sihoni, mfalme wa Waamori,
Na Ogu, mfalme wa Bashani,
Na falme zote za Kanaani.
12 # Mwa 17:8 Akaitoa nchi yao iwe urithi,
Urithi wa Israeli watu wake.
13 # Kut 3:15 Ee BWANA, jina lako linadumu milele,
BWANA, sifa zako zitakumbukwa na vizazi vyote.
14 # Kum 32:36 Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,
Na kuwahurumia watumishi wake.
15 # Zab 115:4-8; Ufu 9:20 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,
Kazi ya mikono ya wanadamu.
16Zina vinywa lakini hazisemi,
Zina macho lakini hazioni,
17Zina masikio lakini hazisikii,
Wala hamna pumzi vinywani mwake.
18Wazifanyao watafanana nazo,
Na kila mmoja anayezitumainia.
19Enyi mlango wa Israeli, mhimidini BWANA;
Enyi mlango wa Haruni, mhimidini BWANA;
20Enyi mlango wa Lawi, mhimidini BWANA;
Ninyi mnaomcha BWANA, mhimidini BWANA.
21Na ahimidiwe BWANA toka Sayuni,
Akaaye Yerusalemu.
Haleluya.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 135: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia