Zaburi 13
13
Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Kum 31:17; Ayu 13:24; Zab 22:1; Isa 59:2 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?
Hadi lini utanificha uso wako?
2Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,
Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?
Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
3 #
Ezr 9:8; Zab 18:28; Lk 2:32; Ufu 21:23; Zab 76:5,6; Isa 37:36; Yer 51:39; Efe 5:14 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;
Uyatie nuru macho yangu,
Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;
Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5 #
2 Nya 20:12
Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako;
Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6Naam, nitamwimbia BWANA,
Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 13: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.