Zaburi 119:89-96
Zaburi 119:89-96 SRUV
Ee BWANA, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi, Umeiweka nchi, nayo imethibitika. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika mateso yangu. Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha. Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza, Nitazitafakari shuhuda zako. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali amri yako haina kikomo.