Zaburi 119:89-96
Zaburi 119:89-96 NEN
Ee BWANA, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni. Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu. Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia. Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu. Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu. Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako. Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako. Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.