Zaburi 119:89-96
Zaburi 119:89-96 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno lako, ee Mwenyezi-Mungu, ladumu milele; limethibitika juu mbinguni. Uaminifu wako wadumu vizazi vyote, umeiweka dunia mahali pake nayo yadumu. Kwa amri yako viumbe vyote vipo leo, maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningalikwisha angamia kwa taabu zangu. Sitasahau kamwe kanuni zako, maana kwa hizo umenipa uhai. Mimi ni wako, uniokoe, maana nimejitahidi kuzishika kanuni zako. Waovu wanivizia wapate kuniua; lakini mimi natafakari masharti yako. Nimetambua kila kitu hufikia kikomo, lakini amri yako ni kamilifu.
Zaburi 119:89-96 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi, Umeiweka nchi, nayo imethibitika. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika mateso yangu. Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha. Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza, Nitazitafakari shuhuda zako. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali amri yako haina kikomo.
Zaburi 119:89-96 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi, Umeiweka nchi, nayo inakaa. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika taabu zangu. Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha. Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza, Nitazitafakari shuhuda zako. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali agizo lako ni pana mno.
Zaburi 119:89-96 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni. Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu. Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia. Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu. Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu. Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako. Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako. Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.