Zaburi 105:16-25
Zaburi 105:16-25 SRUV
Akasababisha njaa katika nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea. Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani. Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma. Hadi wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya BWANA ilimjaribu. Mfalme alituma watu na kumfungua, Mkuu wa watu akamwachilia huru. Akamweka kuwa mkuu wa nyumba yake, Na mwenye mamlaka juu ya mali yake yote. Awaongoze maofisa wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima. Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu. Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao. Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake.