Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 105:16-25

Zaburi 105:16-25 NEN

Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote, naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa. Walichubua miguu yake kwa minyororo, shingo yake ilifungwa kwa chuma, hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la BWANA lilipomthibitisha. Mfalme alituma watu wakamfungua, mtawala wa watu alimwachia huru. Alimfanya mkuu wa nyumba yake, mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo, kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo na kuwafundisha wazee wake hekima. Kisha Israeli akaingia Misri, Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu. BWANA aliwafanya watu wake kuzaana sana, akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao, ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.