Filemoni 1:17-25
Filemoni 1:17-25 SRUV
Basi ikiwa waniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama ambavyo ungenipokea mimi mwenyewe. Na kama amekudhulumu, au unamdai kitu, ukiandike hicho juu yangu. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakudai hata nafsi yako. Naam, ndugu yangu, nifaidi kwa hili katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo. Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana natumaini ya kwamba kwa maombi yenu nitarejeshwa kwenu. Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.