Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Filemoni 1

1
Salamu
1 # Efe 3:1 Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, 2#Kol 4:17; 2 Tim 2:3 na kwa Afia, dada yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako. 3#Rum 1:7 Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Upendo na imani ya Filemoni
4Namshukuru Mungu wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu; 5nikisikia habari za upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote; 6#Flp 1:9 naomba ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo. 7#2 Kor 7:4 Maana nilikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu.
Ombi la Paulo kwa ajili ya Onesimo
8Kwa sababu hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo; 9lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ndimi, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia. 10#Kol 4:9; Gal 4:19; 1 Kor 4:15 Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa nikiwa kifungoni mwangu, yaani, Onesimo; 11ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia; 12niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa; 13#Flp 2:30 ambaye mimi nilitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako, niwapo katika kifungo kwa ajili ya Injili. 14#2 Kor 9:7; 1 Pet 5:2 Lakini sikutaka kutenda neno lolote isipokuwa kwa ushauri wako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. 15Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; 16#1 Tim 6:2 tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. 17Basi ikiwa waniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama ambavyo ungenipokea mimi mwenyewe. 18Na kama amekudhulumu, au unamdai kitu, ukiandike hicho juu yangu. 19#Gal 6:11; 2 The 3:17 Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakudai hata nafsi yako. 20Naam, ndugu yangu, nifaidi kwa hili katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo.
21Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. 22#Flp 1:25; 2:24 Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana natumaini ya kwamba kwa maombi yenu nitarejeshwa kwenu.
Salamu za mwisho na baraka
23 # Kol 1:7; 4:12 Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; 24#Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; 19:29; 27:2; Kol 4:10,14; 2 Tim 4:10,11 na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. 25Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.

Iliyochaguliwa sasa

Filemoni 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha