Filemoni 1:17-25
Filemoni 1:17-25 NEN
Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika wako, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe. Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi. Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa. Sitaji kwamba nakudai hata nafsi yako. Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana, uuburudishe moyo wangu katika Kristo. Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba. Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu. Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu, anakusalimu. Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.