Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 28

28
Sadaka za kila siku
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Law 3:11; 21:6,8; Mal 1:7,12 Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao. 3#Kut 29:38 Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsogezea BWANA; wana-kondoo dume wawili wa mwaka mmoja wakamilifu, kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. 4#Kut 12:6 Mwana-kondoo mmoja utamsongeza asubuhi, na mwana-kondoo wa pili utamsongeza jioni; 5#Kut 16:36; 29:38-42; Law 2:1; Hes 15:4 pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa. 6Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto. 7#Kut 29:42; 30:9; Law 23:13; Hes 15:5-10; Isa 57:1 Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia BWANA katika mahali hapo patakatifu. 8Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Sadaka za Sabato
9Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo dume wawili, wa mwaka mmoja, wakamilifu, pamoja na sehemu ya mbili ya kumi za efa za unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji; 10#Eze 46:4 hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Sadaka za kila siku
11 # Hes 10:10; 1 Sam 20:5; 1 Nya 23:31; 2 Nya 2:4; Ezr 3:5; Neh 10:33; Isa 1:13,14; Eze 45:17; Hos 2:11; Kol 2:16 Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe dume wadogo wawili, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo wa kiume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; 12#Hes 15:4; 29:10; Eze 46:5,7 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng'ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo dume mmoja; 13na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana-kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 14Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng'ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo dume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. 15Tena mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Sadaka za Pasaka
16 # Kut 12:1-13; Kum 16:1-2; Law 23:5; Eze 45:21; Mt 26:2,17; Lk 22:7 Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni Pasaka ya BWANA. 17#Kut 12:14-20; 23:15; 34:18; Kum 16:3-8; Law 23:6 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba. 18#Law 23:7 Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi; 19#Law 22:20; Hes 29:8; Kum 15:21 lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA; ng'ombe dume wachanga wawili, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja saba; watakuwa wasio na dosari kwenu; 20pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya tatu ya kumi kwa ng'ombe mmoja, na sehemu ya mbili ya kumi kwa kondoo dume; 21na sehemu ya moja ya kumi utasongeza kwa kila mwana-kondoo; wale wana-kondoo saba; 22#Law 16:18; Rum 8:3; Gal 4:4; Ebr 9:12; 10:1 tena mtasongeza mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 23Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. 24#2 Kor 2:15; Efe 5:2 Mtasongeza sadaka kwa jinsi hii kila siku kwa muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 25#Kut 12:16; 13:6; Law 23:8 Na siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi.
Sadaka za majuma
26 # Kut 23:16; 34:22; Kum 16:9-12; Law 23:10,15; Mit 3:9; Mdo 2:1 Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsogezea BWANA sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi; 27#Law 23:18,19 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume wadogo wawili, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo wa kiume wa mwaka wa kwanza saba; 28pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng'ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo dume, 29na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba; 30na mbuzi dume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 31Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 28: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia