Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 27

27
Mabinti wa Selofehadi
1 # Hes 14:35; 26:33; 36:1,11; 1 Nya 7:15; Yos 17:3 Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza. 2#Hes 26:64,65; 14:22-37; Rum 5:12; 6:23 Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema, 3Baba yetu alikufa nyikani, naye hakuwamo katika mkutano wa hao waliojikutanisha kinyume cha BWANA katika mkutano wa Kora; lakini akafa katika dhambi zake mwenyewe; naye alikuwa hana wana wa kiume. 4Kwa nini basi jina la baba yetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake baba yetu. 5#Kut 18:15; 25:22; Law 24:12,13; Mit 3:5,6 Basi Musa akaleta neno lao mbele ya BWANA 6BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 7#Hes 36:2 Hao binti za Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao. 8Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume, ndipo binti yake atapewa urithi wake. 9Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake. 10Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake. 11#Hes 35:29 Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Yoshua afanywa kiongozi wa Waisraeli baada ya Musa
12 # Kum 3:23-27; 32:48-52; 34:1 BWANA akamwambia Musa, Panda wewe juu ya mlima huu wa Abarimu, uitazame nchi niliyowapa wana wa Israeli. 13#Hes 20:24,28; 31:2; Kum 10:6; 32:50-52 Na ukiisha kuiona, wewe nawe utakusanyika pamoja na baba zako, kama Haruni ndugu yako alivyokusanyika; 14#Kum 1:37; 32:51; Zab 106:32; Kut 17:7; Hes 20:1,13,24 kwa sababu mliasi juu ya neno langu katika jangwa la Sini wakati wa mateto ya mkutano, wala hamkunistahi, hapo majini, mbele ya macho yao. (Maji hayo ndiyo maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.) 15Musa akanena na BWANA akisema, 16#Hes 16:22; Ebr 12:9; Zek 12:1 BWANA, Mungu wa roho za watu wote, na aweke mtu juu ya kusanyiko,#27:16 Au Mungu wa wanadamu wote. 17#1 Fal 22:17; Eze 34:5; Mt 9:36; Mk 6:34; Kum 31:2; 1 Sam 8:20; 18:13; 2 Nya 1:10; 2 Nya 18:16 atakayetoka mbele yao, na kuingia mbele yao; atakayewaongoza watokapo, na kuwaleta ndani; ili watu wa BWANA wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji. 18#Kut 24:13; Mwa 41:38; Amu 3:10 BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako; 19#Kum 31:7 kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote; ukampe mausia mbele ya macho yao. 20#Hes 11:17; 1 Sam 10:6; 2 Fal 2:15; Kum 34:9; Yos 1:15 Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili jumuiya yote ya wana wa Israeli wapate kutii. 21#Kut 28:30; 1 Sam 14:41; 28:6; Yos 9:14; Amu 1:1; 20:18; 1 Sam 23:9; 30:7; Law 8:8; Kum 33:8; 1 Sam 28:6; 1 Sam 22:10 Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia. 22Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote; 23#Kum 3:28; 31:23; Isa 55:4 kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 27: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia