Hesabu 29
29
Sadaka za sikukuu ya mabaragumu
1 #
Law 23:24; Zab 89:15; Isa 27:13; Zek 9:14; Mk 16:15; 1 Kor 15:52; Ufu 8:6-13 Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu. 2Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja wote wasiwe na dosari; 3pamoja na sadaka yake ya unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi ya ng'ombe, sehemu ya mbili ya kumi kwa kondoo dume, 4na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; 5na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu; 6#Hes 28:11; Kut 29:38; Law 6:9; Hes 28:3; Dan 12:11; Hes 15:11,12 zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto.
Sadaka za siku ya upatanisho
7 #
Law 16:29-34; 23:27; Ezr 8:21; Zab 35:13; Isa 58:5; Mt 5:4; Lk 13:3,4; 1 Kor 9:27; 2 Kor 7:9; Yak 4:9 Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtajinyima nafsi zenu, msifanye kazi yoyote ya utumishi 8#Law 22:20; Hes 28:19; 29:8; Kum 15:21; 17:1 lakini mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja; watakuwa wakamilifu kwenu; 9pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi kwa huyo ng'ombe, na sehemu ya mbili ya kumi kwa huyo kondoo, 10na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; 11#Law 16:3,5 na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
Sadaka za siku kuu ya vibanda
12 #
Law 23:34; Kum 16:13-15; Kut 23:16; 34:22; Eze 45:25 Tena siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote kwenye nafsi zenu, nanyi mtamfanyia BWANA sikukuu muda wa siku saba; 13#Ezr 3:4; Ebr 10:1-18; Dan 9:24; Ebr 7:18; 8:13 nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume wachanga kumi na watatu na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu; 14pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi kwa kila ng'ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya mbili ya kumi kwa kila kondoo katika hao kondoo dume wawili; 15na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo kumi na wanne; 16na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
17Tena siku ya pili mtasongeza ng'ombe dume wachanga kumi na wawili, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne wakamilifu; 18#Hes 15:12; 28:7,14; Law 2:1 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri hiyo; 19na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
20Tena siku ya tatu mtasongeza ng'ombe dume kumi na mmoja, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne; 21pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo kama idadi yao ilivyo kulingana na amri; 22na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
23Tena siku ya nne mtasongeza ng'ombe dume kumi, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne; 24na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri; 25na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
26 #
Yn 1:29; Ebr 7:26; 1 Pet 1:19; Ufu 1:6-14 Tena siku ya tano mtasongeza ng'ombe dume tisa, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne; 27pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri; 28na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
29Tena siku ya sita mtasongeza ng'ombe dume wanane, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne; 30pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri; 31na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
32Tena siku ya saba mtasongeza ng'ombe dume saba, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne; 33pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri; 34na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
35 #
Law 23:36; Zab 47:5,6; Isa 11:10; 54:1; 60:1; Mt 28:1; Yn 7:37; Ebr 1:3; 4:9; Ufu 7:9-17; 11:15; 21:1; 22:1 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yoyote kwenye nafsi zenu; 36lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari saba; 37pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa huyo ng'ombe, na kwa huyo kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri; 38na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
39 #
Law 23:2; 1 Nya 23:31; 2 Nya 31:3; Ezr 3:5; Neh 10:33; Isa 1:14; Law 7:11,16; 22:21; 23:38; Hes 6:21; 7:21; Kum 12:6; 1 Kor 10:31 Sadaka hizo mtamsogezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani. 40#Kut 24:3; Kum 5:27-31; 33:4; Yn 1:17; 7:19; Mdo 7:37,38 Naye Musa akawaambia wana wa Israeli vile vile kama hayo yote BWANA alivyomwagiza Musa.
Iliyochaguliwa sasa
Hesabu 29: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.