Zab 84:5-12
Zab 84:5-12 SUV
Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu. BWANA, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize, Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi wako. Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu. Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.