Zaburi 84:5-12
Zaburi 84:5-12 NEN
Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi. Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni. Ee BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu. Kwa kuwa BWANA ni jua na ngao, BWANA hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia. Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.