Zaburi 84:5-12
Zaburi 84:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri watu wanaopata nguvu zao kwako, wanaotamani kwenda kuhiji mlimani kwako. Wapitapo katika bonde kavu la Baka, hulifanya kuwa mahali pa chemchemi, na mvua za vuli hulijaza madimbwi. Wanaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi; watamwona Mungu wa miungu huko Siyoni. Usikie sala yangu ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi; unitegee sikio, ee Mungu wa Yakobo. Ee Mungu, umwangalie kwa wema ngao yetu mfalme, umtazame huyo uliyemweka wakfu kwa mafuta. Siku moja tu katika maskani yako, ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali kusimama mlangoni pa nyumba yako, kuliko kuishi nyumbani kwa watu waovu. Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu. Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, heri mtu yule anayekutumainia wewe!
Zaburi 84:5-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wapitapo katika bonde la baraka, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulijaza baraka. Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu. BWANA, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize, wako. Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu kwingineko; Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kuishi katika hema za uovu. Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.
Zaburi 84:5-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu. BWANA, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize, Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi wako. Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu. Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.
Zaburi 84:5-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi. Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni. Ee BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu. Kwa kuwa BWANA ni jua na ngao, BWANA hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia. Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.