Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 84:5-12

Zaburi 84:5-12 NENO

Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi. Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni. Ee Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu. Kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu ni jua na ngao; Mwenyezi Mungu hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia. Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, heri mtu anayekutumaini wewe.