Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 143:8-11

Zab 143:8-11 SUV

Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. Ee BWANA, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, Ee BWANA, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 143:8-11