Zaburi 143:8-11
Zaburi 143:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Asubuhi unioneshe fadhili zako, maana nimekuwekea tumaini langu. Unifundishe mwenendo wa kufuata, maana nakuelekezea ombi la moyo wangu. Uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu, kutoka maadui zangu, maana kwako nakimbilia usalama. Unifundishe kutimiza matakwa yako, maana wewe ni Mungu wangu! Roho yako nzuri iniongoze katika njia sawa. Unifadhili, ee Mwenyezi-Mungu, kwa hisani yako, uniondoe katika taabu kwa sababu ya uadilifu wako.
Zaburi 143:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu. Ee BWANA, uniponye kutoka kwa adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa, Ee BWANA, uniponye kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni
Zaburi 143:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. Ee BWANA, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, Ee BWANA, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni
Zaburi 143:8-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. Nionyeshe njia nitakayoiendea, kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. Ee BWANA, uniokoe na adui zangu, kwa kuwa nimejificha kwako. Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare. Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, kwa haki yako nitoe katika taabu.