Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 105:16-25

Zab 105:16-25 SUV

Akaiita njaa iijilie nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea. Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani. Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma. Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya BWANA ilimjaribu. Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia. Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake, Na mwenye amri juu ya mali zake zote. Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima. Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu. Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao. Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake.